Je, majina yetu hayawezi kubeba falsafa zetu?.

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Posts
2,440
Reaction score
2,572
Kuna hili suala la majina yetu. Inafahamika wazi kwamba tunapozaliwa, mara nyingi shughuri ya kwanza kabisa inayofanywa na wazazi au walezi wetu, ni kutupatia majina 'yao' wanaojisikia au/na kuona yatatufaha. Hivyo watoto tunajikuta tukirithi dini za wazazi wetu, bila kuhoji na majina hayo tunayabeba mazima mazima katika maisha yetu.

Majina haya mara nyingi, watoto tunapewa bila tafakari ya kina. Wapo wazazi au/na walezi, ambao wanaamua tu kuwapa watoto wao hayo majina, na wapo wengine wanatembea na sababu mbalimbali kama vile matukio ya wakati huo mtoto alipokuwa anazaliwa, historia ya mtu/kitu fulani n.k....bila kujali ni kwa namna gani mtuto huyo atakavyojisikia, hasa pale atakapo kuwa na uwezo wa kubaini maana au/na historia halisi ya jina alilopewa.

Kwa mfano, mtoto anapoitwa matatizo, masumbuko, shida na majina mengineyo kama hayo. Mtoto huyo anapokuja kubaini kuwa jina alilopewa na wazazi au/na walezi wake alikuwa sahihi kwake, hivyo kuna uwezekano mkubwa ukaleta hisia za ubashiri kwa mtoto huyo, juu ya aina gani ya maisha atakayoishi na hapo ndio mkanganyiko unapoanza.

Wengine hupewa majina mazuri, lakini ya kigeni....yasiyo na utamaduni wetu. Pengine yametokana na dini, sanaa n.k. Mara nyingi tunayafurahia hayo majina, lakini kimsingi yanaweza yakawa kielelezo tosha cha utumwa wa kifikra tulionao. Kumbe majina hayo hayo yangeweza kuwa katika lugha zetu mama na kuonesha kuwa tu watu tunaojiamini, kuheshimu na kupenda utamaduni wetu.

Majina haya tunayowapatia watoto wetu, mara nyingi yanaleta migogoro ya kisaikolojia na/au kiutamaduni. Nadhani kuna haja kamilifu ya kukaa chini, na kuliangalia suala hili kwa upana zaidi. Ikiwezekana watoto watambulike kwa majina ya mpito, mpaka pale watakapojielewa na kuweza kujichagulia majina yao wenyewe, yenye kusadifu falsafa walizonazo.

"Kwanini majina yetu yasingebeba falsafa yetu wenyewe, na wazazi wakabaki kuwa washauri?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…