John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Je Malaika ni Hadithi za Kale au Wapo Hadi Leo
Malaika ni nani
Neno la Mungu huwaeleza malaika kuwa roho wenye uwezo mwingi sana, na roho haionekani kwa macho ya binadamu (1Wafalme 22:21; Zaburi 34:7; 91:11). Biblia husema kwamba, “katika yeye (Yesu), vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana” (Wakolosai 1:16). Yehova Mungu, kupitia Mwanae mzaliwa wa kwanza, si kwamba tu aliumba malaika muda mrefu kabla ya mwanadamu, bali pia aliwafanya wenye umbo la uhai wa juu zaidi kushinda mwanadamu (Ayubu 38:4,7; 2Petro 2:11).
Je Malaika wapo kweli
Malaika aliyemtokea mke tasa wa Manoa, akatangaza kutungwa mimba ya mwanae, Samsoni, alikuwa halisi kwake.
Ndivyo walivyokuwa wale malaika watatu waliomtokea Abrahamu na Sara, mke wake, na wale wawili waliomtafuta Loti, na yule mmoja, aliyeketi chini ya mti mkubwa na kuongea na Gideoni (Mwanzo 18:1-15; 19:1-5; Waamuzi 6:11-22; 13:3-21). Wakati wa kuzaliwa kwa Yesu, malaika alitokea ghafla kikundi cha wachungaji, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu (Luka 2:8-9).
Malaika wa Yehova ndiye aliyeua Waashuri 185,000 katika kambi ya adui wa Israeli kwa usiku mmoja tu (Isaya 37:36). Ni matukio ya uwepo wa malaika.
Je malaika ni wa kiwango cha juu kuliko wanadamu
Malaika ni wa kiwango cha juu kuliko wanadamu (Zaburi 8:4-5): "Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? umemfanya mdogo punde kuliko malaika; umemvika taji ya heshima." Malaika wanaweza kutokea katika mfumo wa watu wa kawaida (Waebrania 13:2): "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua." Malaika walipojionyesha kwa binadamu, siku zote walitokea kama wanaume waliovishwa nguo kabisa, si kama wanawake au watoto, na hawakutokea kamwe kama binadamu nusu.
Malaika wana kazi gani
Neno malaika linatokana na neno la Kigiriki aggelos (au angelos), ambalo humaanisha “mjumbe.” Katika Agano la Kale la Kiebrania, viumbe hawa wanaitwa mal’ak ambalo linamaanisha kitu kile kile “mjumbe”. Katika Biblia, mawasiliano yaonekana kuwa kazi kuu ya malaika. Marejeleo mengi inawahusisha wao kutoa habari au amri kwa niaba ya Mungu. Mara kwa mara wanaoneshwa kuwa walinzi wa watu fulani (Danieli 6:20-23) au mataifa (Danieli 12:1). Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu (Waebrania 1:14).
Malaika watakuondoa kwenye shida (Zaburi 34:7): “Malaika wa bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamshao na kuwaokoa". Malaika hutulinda (Zaburi 91:10-12): "Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitakaribia hema yako. kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote." Malaika huchukua na kutekeleza amri za Mungu (Zaburi 103:20-21): " Mhimidini Bwana enyi malaika zake, ninyi mlio hodari mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini Bwana, enyi majeshi yake yote, ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake".
Malaika hulieneza neno la Mungu (Luka 2:9-10): "Malaika wa Bwana akawatokea ghafla utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote wakaingiwa na hofu kuu malaika akawaambia msiogope; kwa kuwa mimi nimewaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote".
Malaika watakuwa na kazi gani atakapo kuja yesu mara ya pili (Mathayo 16:27): "Kwa sababu mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake". "Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu mbingu mpaka mwisho huu" (Mathayo 24:31).
Kuna malaika wangapi mbinguni
Biblia haijatoa idadi kamili ya malaika Mungu aliowaumba. Inatumia neno MAJESHI, ambayo majeshi yenyewe hayo yapo maelfu kwa maelfu. Waebrania 12:22: “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na MAJESHI ya malaika ELFU NYINGI”. Ufunuo 5:11: “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu”. Vifungu kadhaa vya maandiko vinaelezea malaika kuwa ni wengi kama nyota (Ufunuo 12:4, Ayubu38:7, Danieli 8:10, Waamuzi 5:20).
Malaika wana mipaka ya kazi zao
Malaika wana mipaka pia. Mambo fulani ya hakika juu ya Kristo na wakati ujao yalifunuliwa kwa manabii na wanadamu, wala si kwa malaika. Neno la Mungu hutuambia kwamba ni katika “mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia” (1Petro 1:10-12). Kwa habari ya tarehe barabara iliyochaguliwa na Mungu ya kuja kwa Bwana, Yesu alisema: “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake” (Mathayo 24:36).
Malaika wapo wa aina ngapi
Wapo malaika wa sifa: Hawa wapo mbele za Mungu usiku na mchana kuilinda enzi yake, ndio wale Maserafi na Makerubi; ambao tunawasoma kwenye: Ezekieli 1:4-28, Isaya 6:2-6.
Wapo malaika wa vita: Mfano wa hawa ni Mikaeli na malaika zake: 2Wafalme 6:17, Ufunuo 12:7, Yeremia 5:14, 38:17, Hosea 12:5.
Wapo malaika wa ujumbe: Mfano wake ni Gabrieli: Danieli 8:16, 9:21, Luka 1:19, 26.
Wapo malaika wa vitu vya asili tu: kama vile moto, maji: Ufunuo 14:18, 16:5.
Wapo malaika wa ulinzi, (miji na mataifa): Danieli 4:13.
Wapo malaika wa ulinzi (wanadamu): Mathayo 18:10, Zaburi 34:7.
Wapo malaika wa huduma (watumishi): Matendo 5:19, 7:30, 8:26, 12:15, 27:23, Waebrania 1:14.
Wapo malaika wa mapigo: Zaburi 78:49, Ufunuo 16.
Wapo malaika wa uponyaji: Yohana 5:4, Isaya 6:7.
Pamoja na hao, wapo pia malaika walioasi, ambao biblia inatuambia walikuwa ni theluthi ya malaika wote waliokuwa mbinguni. Na hao idadi yao haihesabiki, katikati yao kuna ambao wapo vifungoni, wanasubiri hukumu ya mwisho (Yuda 1:6). Wengine wapo vifungoni lakini watakuja kuachiliwa kwa muda kidogo wafanye kazi duniani kwa muda mfupi kisha wataondolewa (Ufunuo 9:1-11), na wengine wapo bado hapa duniani wakizururazurura tu kuwaharibu watu, na kusababisha maovu duniani.
Tunaona kuwa Mungu aliumba malaika muda mrefu kabla ya mwanadamu. Wapo hadi leo na hadi milele. Ni viumbe halisi na hai. Ni roho wenye uwezo mwingi sana kuliko wa mwanadamu. Malaika wanaweza kutokea katika mfumo wa watu wa kawaida. Malaika hutoa habari au amri kwa niaba ya Mungu. Mara kwa mara wanaoneshwa kuwa walinzi wa watu fulani. Wako kwa idadi ya elfu nyingi. Hesabu yao inatajwa kuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu. Malaika wapo wengi kama nyota.