Je maliasili imebadili Sheria faini za pikipiki?

Je maliasili imebadili Sheria faini za pikipiki?

boseboi

Member
Joined
Jan 22, 2025
Posts
18
Reaction score
64
Habari zenu ndg jamaa, naomba kuuliza kama Kuna mwenye kujua, nilikua najishughulisha na biashara ya kubeba mkaa hapa mkoan Dodoma katika mihangaiko yangu mwaka Jana mwezi wa na Nne tulikamatwa na maliasili Mimi na mwenzangu tulikua wawili.

Mwenzangu pikipik ili kua mpya hata week hajamaliza akaifatilia pale wakamzungusha kama week ivi baadae akapewa control namba akaenda akalipia laki nne akapewa pikipik, upaande wangu mambo yalikua mengi nikawa sina ela nikaona ngoja ikae kwanza nikaanzisha biashara nyingine.

Mwezi uliopita nikaenda Sasa nikaitoe kwenye ofisi zao ndogo pale nane nane nikakuta, mabadiliko kidogo mwanzo pale walikua wapo Suma jkt na ma afisa maliasili wachache ila nilivoenda awam hii nikakuta wapo jkt wenyewe na wakasema faini ni million Moja si laki nne kama aliotoa mwenzangu na customer care Yao si ya kuridhisha, nikajiondokea, asa naomba kuuliza maliasili hua wanauza pikipik zilizokaa muda mrefu kwamba itakua imeshauzwa au ni kweli faini imepanda?
 
Back
Top Bottom