Hili ni swali linalofikirisha watu wengi sana kipindi hiki ambapo homa ya Uchaguzi inazidi kupambamoto. Swali hili linakuja baada ya wajumbe wengi wa CCM kuamua kwa maksudi kupuuza makatazo na maagizo ya chama na viongozi wake. Maeneo mengi nchini wajumbe wa CCM wakiwemo viongozi wa chama ngazi ya Wilaya wanalaumiwa Sana kwa kupiga kura zao kwa kuangalia nani kawapa rushwa nono na sio kwa mujibu wa sifa na uwezo wa wagombea na maoni ya Wanachama/wananchi wa kawaida.
Kwa muktadha huo, maeneo mengi, wanachama/wananchi wa kawaida wamewatupia lawama wajumbe kwa kupigia kura Watia Nia wasio na sifa wala uwezo wa kuwakilisha wananchi. Kwenye baadhi ya maeneo, wajumbe wamerudisha wagombea ambao walikuwa wanalalamikiwa Sana na wananchi kuwa ni wabunge/madiwani goigoi na wasio sifa wala uwezo wa kuwawakilisha vyema.
Wananchi/wanachama wa kawaida wanatamani Sana vikao vya juu vya chama viwaulize wananchi wa kawaida ni nani wanaona anafaa kuwa mgombea wao kwani maeneo mengi wananchi wa kawaida wamekatishwa tamaa na maamuzi ya wajumbe na hawakubaliani na kile walichokifanya wajumbe.
Kwa kuwa muda wa kuuliza wananchi/wanachama wa kawaida unaweza usitoshe; je,unashauri nini kifanyike ili CCM iweze kupata wagombea wenye mvuto, uwezo na sifa za kukabiliana kikamilifu na wagombea wa upinzani?