Wakubwa, mkopo ni sehemu ya biashara yoyote ile. Tatizo linaloikumba America leo ni viongozi vijana ambao sio wanasiasa ambao wameshinda na wamesema wanakuja kukomesha tabia ya ukopaji ya America. Vijana hawa maarufu kama Tea Party sio career politician, bali ni watu wenye idea za mlengo wa kulia. Wamekataa kuipa serikali ya Obama uwezo wa kukopa zaidi ya kiwango cha sasa, unless Obama akate matumizi sawa na kiwango anachotaka kuongeza kukupa. Maana Moja toa moja.
America inapita kwenye wakati mgumu kama ilivyokuwa miaka ya themanini, jee inaweza kurudi na kusimama? I guess yes, lakini mengi inabidi yafanyika na moja wapo ni KUMTOA Mkenya madarakani sababu hajui anachofanya.
China ina Population mara 4 ya Marekani, lakini America ina uchumi twice wa China, sasa wewe kama unajua hesabu angalia nani ana stronger economy hapo. Pili USA ananunua almost 30% ya output zote zinazo zalishwa china, so China can't afford weak US economy.