Je, Marekani kuanza kusitisha baadhi ya misaada kutaathiri Demokrasia katika nchi za ulimwengu wa tatu ikiwepo Tanzania?

Je, Marekani kuanza kusitisha baadhi ya misaada kutaathiri Demokrasia katika nchi za ulimwengu wa tatu ikiwepo Tanzania?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Mpo salama wote!

Awamu ya pili ya Donald Trump imekuwa na Sera korofi kwa mataifa mengine. Sera ya isolation ni Sera ambayo nchi Fulani hujitenga na mataifa mengine na kufungia Fursa za kiuchumi ndani ya taifa husika.

Tunajua kuwa Demokrasia ilianzia nchi za Ulaya hasahasa nchi ya Ugiriki kisha baadaye Kupata nguvu katika nchi za Ulaya Magharibi kama Uingereza, ujeruman na ufaransa.

Baada ya vita ya Pili ya Dunia, na kuibuka kwa taifa la Marekani kama taifa Kubwa na kiranja WA Dunia. Taifa Hilo liliamua kuitumia Demokrasia kama Fimbo na silaha kwa mataifa mengine ambayo hayakuwa na utamaduni wa demokrasia.
Kwa Marekani Demokrasia ingekuwa Sera ya lazima na silaha muhimu ya kukabiliana na mataifa mengine hasa ya Afrika, America ya Kusini, na bara la Asia.

Ni kupitia Demokrasia Marekani huwa na nguvu kwa mataifa mengine kwani ndio Njia rahisi kupenyeza vibaraka wake.
Hii ni kusema, Demokrasia ni kama king'amuzi cha kudhibiti mataifa mengine kisiasa huku viongozi wa mataifa hayo wakitumiwa kama Rimoti tuu.

Umaskini, fikra za Giza, ujinga, Mila na desturi kandamizi ambazo zilitawala Afrika na nchi za ulimwengu wa tatu zilifikia katika ukingo. Tamaa na shauku ya watu kuiona Nuru na kuondokana na Umaskini, utumwa na ukoloni vilizidi kumea na kustawi miongoni mwa Waafrika.

Lakini namna ipo,mikakati ipi, Mbinu ipi zitumike, hicho kilikuwa kitendawili.
Tutawezaje kujikomboa na Umaskini huu tungali hatuna pesa, teknolojia na tuwajinga?

Wazee hawakuwa na namna zaidi ya kukimbilia Misaada.
Na hapo ndipo Marekani na Washirika wenzake walipotumia silaha Zao za kimifumo kutudhibiti.

Ili tuwape Misaada mtapaswa mtumie Demokrasia katika mifumo yenu ya uongozi na kisiasa.
Zingatia, Marekani haikujengwa na Demokrasia, Uingereza, ujerumani, ufaransa, Ubelgiji, ureno na mataifa makubwa yote hayakujengwa na Demokrasia.

Ni baada ya mafanikio ndipo Demokrasia iliasisiwa. Demokrasia haiendani na watu wajinga, Maskini na watu wenye njaanjaa.

Swali Linakuja,
Je Marekani kupunguza Misaada yake itaathiri Demokrasia katika mataifa ya ulimwengu wa tatu?

Maiki kwenu!

Mtibeli, Safarini,
 
Sasa hivi hawezi kutupangia hata kama tukitembeza rungu kuanzia october, hatuna reciprocal commitment ya demokrasia kwa misaada ya maendeleo
 
Back
Top Bottom