Je, Matumizi ya kila siku ya Fridge, Blender, Pasi, Jiko la umeme n.k naweza vuka units 75 kwa mwezi?

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Za jioni ndugu, nahamia sehemu, na sababu ni nyumba mpya Umeme Bado haujaunganishwa na zero taarifu, ila lengo langu nikitimiza masharti basi niunganishiwe ili niweze kuchezea kwenye units 75 kushuka maana nimesikia ndio kiwango cha juu kuunganishwa na zero taarifu.

Nilikotoka nilikua nimepanga, kwahio hata umeme ni wa share sikuweza ku calculate,

Sasa nitaanza kujitegemea, jee kwa watu wawili
Nikiwasha Fridge, Kupasi nguo asubuhi, Kutumia heater kupasha maji, Natumia jiko la umeme japo mara chache, Taa, Tv, radio, blender, breakfast Maker...
Je naweza fikisha pengine hata kuvuka matumizi ya units 75 kwa mwezi?

Kwa ufupi nina vifaa vingi vya umeme ila vya mara kwa mara ni hivyo, swali langu jee naweza kutumia units 75 kwa mwezi?
NOTE: vifaa vyangu vyote ni energy efficient.

Swali jingine la ziada, vigezo/taratibu za kuunganishiwa zero taarifu vipoje?
Na je katika zero taarifu 1,000tsh = units ngapi?
 
Jibu ni ndiyo utavuka!
Fridge kwa siku linakula wastani wa unit 4~6 maanake kwa siku 10 litabugia unit 40KWH, kwa mwezi litabwia unit 120KWH,
Hapo hujaweka taa, TV, brenda, pasi na radio.
Ukiweka na jiko la umeme ndo kabisaa utalia kwa siku linakula unit 1.5~2kwh likiwa jipya, kwa mwez unit 60, ukijumlisha unakaribia unit 200 kwa mwez

Hata ikitokea Tanesco wakate umeme lazima tu huku na huku utavuka unit 100kwh kwa mwezi hata. Ujibane vip

CASE CLOSED MAJIBU NDO HAYO JIPANGE
 
Zero tarif hua napata unit 65.6 kwa 8,000 hua nabalance sana na natoboa mwezi mzima.
Ila unatakiwa uwe na nidham sana ya matumizi ya umeme ukiyumba kidogo unapituliza.
Natumia pasi,friji ndogo hua awasha pale inapohitajika sio nawasha kutwa nzima hata kama hakuna kitu. Kama sipo nazima nikijua kwa kua haifunguliwi haiwezi poteza baridi
Natumia brenda
Tv$ radio erc
Rice cooker.
Sina jiko la umeme wala heater..
 
Kwa matumizi yake lazima avuke tarif 0 ukigusa jiko na heater ni hatari
 
Kwa matumizi yake lazima avuke tarif 0 ukigusa jiko na heater ni hatari
Taarif 4 inafaa watu wasiyo kuwa na fridge na wenye matumizi mepesi na taa zisizozidi 10 !
Zaidi zaidi inafaa zaidi huko kijijini hawana mambo mengi kama feni, heater na fridge!
 
Twende na uhalisia , atuambia kila kifaa kina Wat ngapi ili tupige hesabu hapa tujue kwa mwezi atatumia umeme kiasi gani
 
Chukulia mfano kile kifridge kidogo kabisa cha mlango mmoja huwa kina watt 170w!
Kwa maana hiyo kwa saa moja kinabwia 0.17kwh, kwa masaa 12 kinakula unit 2.04kwh, kwa SAA 24 kinakulia Unit 4.08KWH
Haya ndo mahesabu halisi ya friji mkuu ni kati 2 hadi 4.5KW
 
Kuna rafiki yangu wamepanga wa 5 kwenye nyumba anasema wao kwa mwezi wanatumia umeme wa elf 4..

Hio suala nimekataa na sintokuja kuamini, labda kama huo umeme wanachajia simu tuu au Wanaiba, na nimemtishia kumshtaki Tanesco.
 
Taarif 4 inafaa watu wasiyo kuwa na fridge na wenye matumizi mepesi na taa zisizozidi 10 !
Zaidi zaidi inafaa zaidi huko kijijini hawana mambo mengi kama feni, heater na fridge!
Nina taa 6 frij ya mlango 1,Pasi,brenda, na tv Tuu natumia unit 65 kwa mwezi. Nipo tarif 0
 
Unitt200 hafiki
 
Unit 75 zibaki kwa bachelors, spinsters na wakazi wa vijijini.

Kinyume na hapo, ni kujibana kwa hali ya jiwe kabisaa
 
Unit 75ndogo sana hata km ungekuwa -0 bado ni ndogo
 
Umeetia chumvi sana mkuu nina friji , pasi,brenda na tv natumia unit 16.4 kwa week sawa na unit 65.6 kwa mwezi kwa sh 8,000. Sema matumiszi ndo shida unaweka maji lita 2 unawasha usiku kucha ...unaaliacha mchana kutwa linanguruma lazima lile sana.
 
Chukulia mfano kile kifridge kidogo kabisa cha mlango mmoja huwa kina watt 170w!
Kwa maana hiyo kwa saa moja kinabwia 0.17kwh, kwa masaa 12 kinakula unit 2.04kwh, kwa SAA 24 kinakulia Unit 4.08KWH
Jokofu ni "AC" siyo "DC" kuna wakati inazima yenewe
 
Umeetia chumvi sana mkuu nina friji , pasi,brenda na tv natumia unit 16.4 kwa week sawa na unit 65.6 kwa mwezi kwa sh 8,000. Sema matumiszi ndo shida unaweka maji lita 2 unawasha usiku kucha ...unaaliacha mchana kutwa linanguruma lazima lile sana.
Ukiwa unazima zima ndo kama wewe!
Mimi nimeeleza kwa matumizi FULL TIME, Kuna watu wananunua mboga za wiki au mwezi mzima, kwahiyo fridge mda ote inatakiwa iwe on
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…