Je Mbeya ndiyo chimbuko la hiphop hapa Tanzania?

Je Mbeya ndiyo chimbuko la hiphop hapa Tanzania?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habarini. Si ku nyingi nimekuwa naona wasanii waanzilishi wa hiphop hapa Tz walikuwa wanatokeo, au hasa waliowahi kuishi Mbeya. Sugu anatajwa kama watu wa mwanzo kuanza kuimba hiphop Tz. Huyu ni mzaliwa na mkazi wa Mbeya kabisa.

Kuna mtu kama Prof J, Advance kasoma shule ya Lutengano Mbeya. Jay Mo amesoma Mbeya Irambo. Kuna mstari alisema "Irambo hakuna Tuition." Hiyo Irambo tulikuwa tunasema shule ya watukutu, ipo Mbeya. Kuna Solo Thang ambaye nasikia alisoma shule ya sekondari Sangu.

Nimepita uzi hapo juu unazungumzia historia ya muziki wa Bongo fleva. Jamaa aliyeandika hapo juu, ambaye ni muasisi wa neno Bongo Fleva anasema alisoma Mbeya, yeye pamoja na member wa kundi la kwanza Unit, moja ya makundi ya mwanzo kabisa ya hip hop bongo.

Haya yananifanya niamini hip hop tz ilianzia Mbeya. Hip hop tz ilianzia wapi?
 
Kwa hivyo mziki mmoja una machimbuko mawili?
gVPu2HQT_400x400.jpg
 
Back
Top Bottom