Je, Mbwana Samatta karejeshwa Taifa Stars kwa Shinikizo, Uwoga, Unafiki au kwa sasa Kiwango chake Kimeimarika huko aliko?

Je, Mbwana Samatta karejeshwa Taifa Stars kwa Shinikizo, Uwoga, Unafiki au kwa sasa Kiwango chake Kimeimarika huko aliko?

Huyu ni Mchezaji mwenye Mafanikio Zaidi Kisoka Tanzania kuliko Wote Waliowahi Kutokea katika nchi Yetu mpaka sasa...!

Issue ya Mzee Wake kufura tumsamehe tu, ndio Wazazi wetu Hawa ,ndio ujue damu huwa mzito kushinda hekima..! Aliongea tu baada ya kuwa evoked na emotions.

Samata tunampenda tu na Msuva aitwe pia
 
Samatta ndie mchezaji ghali na mzoefu zaidi bongo, kuwepo kwake uwanjani huleta hamasa kubwa kwa wachezaji wengine na hofu kwa timu pinzani.

Hata asipofunga haina shida kazi yake nzuri huwa ni kuforce kuipandisha juu timu. Jukumu hilo hajawahi kuliacha.

Huyu Samatta bado anahitajika sana taifa Stars hasa katika kupandisha morali ya timu. Binafsi nampa Morocco maua yake.
 
Pamoja na Samata kuonekana Yuko ukingoni mwa soka lake lakini ukweli uliopo hatuna mchezaji ambaye anaziba nafasi yake.
Ni Bora kuendelea kua naye kwakua hatupungukiwi kitu kuliko kuto kuwepo kabisa.
 
Back
Top Bottom