Hivi Mbinguni unakuchukuliaje kwa mfano?.Unajua mijitu mieusi sisi ni mijinga sana tunamuamini mtu mazima na tupo tayari kudanganywa,Kwamba Mwakasege hana Mapungufu ya Kibinadamu?,Ikiwa anayo sasa huko mbinguni ataendaje na kisha kurudi ili hali imeshaandikwa kuwa "Kamwe hakuna kinyonge chochote kitakachoingia huko..."?!!Ufunuo 21:27.Jamani msilete mzaha na Mbinguni nyie.
Sent from my V1901A using
JamiiForums mobile app
Ni kweli ndugu. Ujinga ni mbaya sana, lakini si Sheria kuwa Mwafrika awe mjinga. Maadam unajua kusoma na kuandika, wekeza kila dakika yako utakayokuwa free kwa kusoma Biblia na vitabu mbalimbali. Uzuri mmoja mambo ya kiroho ni very practical. Usikubali tu kwa kuwa mtu kasema, naam, na usivikubali ikiwa havikubaliani na Neno la Mungu.
Kuna mengi yaliyoandikwa kwenye Biblia ambayo kama Wakristo wangeweza kuyaishi kama ilivyoandikwa, "wangeubadilisha" ulimwengu kwa dakika chache sana.
Na ni kweli Mbinguni hakitaingia kilicho kinyonge. Lakini ujue kuwa mtu aliyempokea Yesu Kristo si "kinyonge" tena, bali Mungu amtazamapo, anamwona kama amwonavyo Yesu.
~ "... Yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja Naye" 1Kor. 6:17
~ "... kama Yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu" 1Yohana 4:17
Unasemaje kwa habari ya Isaya?
Isaya 6:1-7
Na Paulo je?
"Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata miaka kumi na minne... Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo...ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene." 2Kor. 12:2-4
Umeona hiyo? Paulo alifanyeje? Alinyakuliwa mpaka wapi? Mbingu ya tatu. Lakini usifikiri alinyakuliwa akiwa ndani ya mwili. Alitengana na mwili wake kwa muda.
Wasomi wa Biblia wanalihusisha hilo tukio na kipindi Paulo alipopigwa kwa mawe kisha akaachwa ikiaminika kuwa alishakufa, na inawezekana ndivyo ilivyokuwa. Lakini"waliomwua" walipoondoka, "akafufuka" na kusimama.
Mimi sikusikia alichosema mtumishi wa Mungu Mwl. Mwakasege. Lakini najua kuwa inawezekana mtu kutoka kwenye mwili wake, kwamba, roho yake ikaiacha mwili na kisha kusafiri mpaka eneo fulani na kisha kurejea kwenye mwili wake. Hata humu Jamii Forum kuna mada inayoongelea jinsi ya kutoka kwenye mwili. Sasa hiyo ni ya kibinadamu, na ni kinyume na Maandiko, ninaamini.
Lakini Mungu akitaka mtu aende Mbinguni au kwingineko kabla ya kufa, hawezi kushindwa kufanya hivyo. Hata Yohana alipokuwa kule kwenye kisiwa cha Patmo, alishaenda mpaka Mbinguni na kurudi. Hakuwa amekufa. Kilichoenda si mwili wake, bali roho yake.
Na ujue, mtu ni roho, na mwili wake ni makazi yake ya hapa duniani. Akifa, anauacha mwili na roho inaenda inakostahili. Ndicho kinachotokea mtu anapokufa. Roho yake hutengana na mwili wake.
Kwa hiyo, inawezekana Mwakasege alishapata experience kama hiyo ya mwili na roho kutengana kwa muda kwa kusudi maalum.