Je, Mchungaji Kumuyi wa Nigeria ameanguka kiroho?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Ni Pastor mkubwa wa kanisa kubwa la kilokole kule Nigeria linaitwa Deeper Life, anasifika kwa kuhuburi injili ya utakatifu na kuishi maisha matakatifu.

Mwanzoni kulingana na baadhi ya shuhuda za watu inasemekana yeye ni mtumishi wa kweli wa Mungu, ila siku hizi mbili tatu nimeona picha zake mtandaoni alivyo kule India na watu anaoanza ku- associate nao, mmh.

Sina uhakika sana na online media news, kama ni kweli ameanguka, mmh nimeshangaa!
 
Weka huo umajinuni wake anaoufanya huko India 🇮🇳
 
mapastor wengi siku hizi wamepoa sana ili hali mwanzo walikuwa moto mkali. Ukiwauliza imekuaje wamepoa wanakujibu Mungu tu ndiye atakayehukumu.
 
Simjui lakini kama alikuwa anahubiri sana mambo ya kidunia kwa waumini wake kama mafanikio ya mali kazi ndoa miujiza etc juwa mission yake imekamilika sasa anakaa anakula alivyochuma.

Wahubiri wanaokaza sana kuhubiri mafanikio ya kidunia bila kutoa maonyo ya dhambi wengi ni wapigaji wapo kukusanya sadaka za mafala lengo likitimia wanarudi kwenye maisha yao halisi.
 
Tutaaminije hii habari bila picha, au ni umbea tu umetoka nao huko kwenye vikoba
 
Mahubiri yake yote tangu mwanzo ni kwenye kuishi maisha ya utakatifu Saint Anno II
 
Ukikaa ndani ya maisha matakatifu kwa muda mrefu utaona mabadiliko mengi ya ajabu. Ukiacha wokovu kwa muda mrefu kisha urudi utaona ulipoacha kulikuwa kuna utakatifu kuliko sasa. Kama kuna mwongofu alikufa miaka mingi halafu afufuke atashangaa kuona wongofu wa sasa walivyo. Siku hizi dhambi hazijulikani ni zipi waumini wanaziparamia bila hofu yeyote na dhamiri zao haziwahukumu
 
Hizi picha zina tatizo gani? Akili yangu imegoma kuvumbua kitu. Hao alio nao wana tatizo gani?
Kusikiliza mziki wa nitongoze alioimba diamond na rayvanny kuna tatizo gani? Kuangalia filamu ya prison break, game of thrones, kusikiliza miziki ya Jay z, Rihanna na Celine Dion kuna tatizo gani? Demi
 
Hakuna tatizo mkuu😀
 
kwa mwongofu haifai kusikiliza miziki ya kidunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…