vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Young Africans kesho watakuwa nchini Afrika kusini kurudiana na timu inayoogopewa kwa Afrika kwa ubora walionao sio wengine ni Mamelodi Sundowns. Kuelekea mechi ya kesho kocha wa Yanga amestua press kwa kuongea maneno yasiyotarajiwa na wengi.
Wengi walitegemea kuona Aucho, Yao na Pacome wangerejea kucheza hiyo mechi. Mamelodi wamekuwa ni moja ya timu yenye bahati kwa kujipima na Yanga bila ya utimamu wa kikosi chao kamili (first eleven) kwa maneno ya kocha huenda kwenye mechi ya kesho wakacheza wale wale au akaingizwa mchezaji mmoja tu katika wale waliokuwa na majeruhi.
"Tunasubiri kuona itakavyokuwa leo kwenye mazoezi ya mwisho, tunaweza kumpata mchezaji katika wale waliokuwa majeruhi.
Ni kweli tunaiwaza nusu fainali ya CAF lakini tunajali pia na usalama wa afya za wachezaji wetu pia. Young Africans haichezi mashindano haya peke yake" Miguel Gamondi