Uchaguzi 2020 Je, Membe atapunguza kura za CCM au za CHADEMA?

Uchaguzi 2020 Je, Membe atapunguza kura za CCM au za CHADEMA?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa 2015 Lowassa alipunguza kura za CCM na hivyo CHADEMA kufaidika.

Mwaka huu ACT wazalendo ina mgombea urais mwenye nguvu zaidi ya yule wa 2015 naye akitokea CCM mh Bernad Membe.

Tunajua kwa rekodi ya 2015 CCM tayari ina mtaji wa kura zaidi ya milioni 8 na CHADEA ina zaidi ya milioni 6 lakini wapiga kura wa mwaka huu 2020 ni milioni 29 na ushee.

Je, uwepo wa Membe kwenye ballot paper utaiumiza CCM au CHADEMA?

Maendeleo hayana vyama!
 
Membe ni special agent kwenye uchaguzi huu, mission kubwa aliyopewa ili apewe ubalozi mwakani ni kuzigawa kura za Lisu into pieces.
sasa mbona anazigawa kura za ccm tu, yani ccm wamekubali kupotea kweli siku ya kufanyani
 
Membe ni special agent kwenye uchaguzi huu, mission kubwa aliyopewa ili apewe ubalozi mwakani ni kuzigawa kura za Lisu into pieces.
Kwakweli huyu jamaa analake jambo nyuma ya pazia. Maalim akae nae kwa umakini sana. Mipango yote wanayopanga usiku unaweza kuta inatua mezani ikulu kabla hata jogoo hakawika mara moja alfajiri
 
Lengo la Magufuli ni kurudisha mfumo wa chama kimoja baada ya utawala wa Kigali model kugota.
 
1. Hatopata kura nyingi. Kama ilivyokuwa kipindi cha CUF huko nyuma, atapata kura nyingi kusini. Awamu ya pili ya JK, Slaa alimzidi JK japo kura nyingi za kusini zilienda kwa Lipumba.

2. Kura za Membe zinapunguza kote kwa Tundu Lissu na kwa Magufuli. Ila Lissu upande wa Lindi na Mtwara atapata kura nyingi kumzidi Magufuli, sababu ya sinema ya korosho.
3. Mikoa mingine yote iliyobaki, Tundu Lissu atamzidi Magufuli.
4. Upande wa Zanzibar, ACT wanfuata Maalim anasema nini. Unguja kura zao nyingi zitaenda kwa Lissu. Hivyo upande wa ZNZ Lissu na Membe watapata kura nyingi kuliko Magufuli.
5. Kitaifa, mshindi wa kwanza atakuwa Tundu Lissu, wa pili Magufuli, wa tatu Membe.
6. Tume itatangaza kwamba mshindi ni Magufuli.
 
Niswali la msingi membe kiuhalisia membe atapunguza kura za ccm nakura hizi nizile za Wana ccm waliochooshwa na chama chao lakini hawaipendi chadema,hata hivyo nivigumu Sana kupunguza kura za chadema kwani kipimo kikuu chakupunguza au kuongeza kura za chadema ni mafanikio chanya ya ccm au kuferi kukidhi matakwa ya wananchi ktk uchumi, elimu,ajila,kilimo na masoko,Kodi shirikishi nk, ukiwa chama uliyepewa dhamana unaweza punguza kura zaidi naunaweza kuongeza zaidi endapo tu haya Mambo utayafanya kwa ufanisi, kutokana na swali lako kura za chama Cha upinzani zinapunguzwa na chama kilichopo madarakani.
 
Mlichowafanyia kwenye korosho kule kusini lazima kura zenu CCM zipungue, wale jamaa wana hasira na nyie.
 
Kura milioni 29 ni hesabu ya NEC na CCM yake kufanikisha wizi wa kura kupitia vituo hewa. Taifa lolote huwezi andikisha zaidi ya nusu ya raia kupiga kura. Watoto ni zaidi ya nusu ya raia wote, na kuna kundi kubwa la watu wazima halina habari na mambo ya uchaguzi, eg vikongwe, wagonjwa nk.
 
Member atapata kura zake anazostahili kama mgombea. Hatapunguza kura za mgombea mwingine. Ila tume ndio itachukuwa za Lisu na Membe ikampa Magufuli na kumtangaza mshindi.
 
Back
Top Bottom