Je mfanyakazi wa serikali anaruhusiwa kwenda tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA)?

Je mfanyakazi wa serikali anaruhusiwa kwenda tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA)?

kimpango

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2011
Posts
600
Reaction score
717
Wanasheria Yamemkuta Ndugu Yangu Muajiriwa wa zamani wa Tanroads Pwani, alifukuzwa kazi kwa makosa yasiyo na kichwa wala kutofuata taratibu akafungua shauri CMA kibaha mwaka unaisha sasa , sasa wakiwa kwenye stage za mwisho baada ya upande wa pili kumaliza kutoa ushahidi wake mlalamikiwa(Tanroads Pwani) ameweka pingamizi (P.O) akisema the case is prematurely before this honorable commission as the complainant being a civil servant under one of The Government Agency was supposed to exhaust all local remedies ...so the case was supposed to be in tume ya utumishi wa uma ikishindikana ndio CMA
Naombeni position ya sheria kwenye hili
kina
Petro Mselewa
Dragoon
Soskeneth
Na wengine wote wataalamu wa sheria
 
Mfanyakazi wa Serikali anaajiriwa chini ya Public Services Act na Its regulation, ndo kuna tume na kamisheni zimeanzishwa huko!
 
OK JIBU SWALI
Kwa hayo maelezo yako alitakiwa kwenda kukata rufaa kwa kamisheni ya utumishi wa umma,akishindwa hapo anakata rufaa kwa Rais ambaye kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu utakua ni uamuzi wa mwisho yani FINAL.Akiwa hajaridhika hapo aende mahakama kuu na kufanya Judicial Review! Hamna kwenda CMA kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu,as long as huyo mtu ni mfanyakazi wa umma,yani Public servant!!
 
SO P O ATASHINDWA
Ndugu yako alikosea utaratibu kama alikuwa mtumishi wa umma alipaswa akate rufaa kwa Katibu Tume ya utumishi wa umma then kwa rais ikishindikana huko ndio alipaswa kwenda mahakama kuu division ya kazi.
 
Inategemea na kinachodaiwa na huyo mtumishi..

Kama alipewa barua ya kufukuzwa kazi basi alichotakiwa ni kukata rufaa hiyo tume ya utumishi wa umma lakini kama amefukuzwa kimyakimya (yaani kaona tu hapati mshahara) bila kupewa barua anatakiwa kwenda CMA kudai mishahara yake na sio kulalamika kuhusu kufukuzwa kazi...

Kwa maelezo uliyotoa kama ni kweli alipewa barua basi njia ilikuwa ni kukata rufaa tume ya utumishi wa umma..
 
Kwa hayo maelezo yako alitakiwa kwenda kukata rufaa kwa kamisheni ya utumishi wa umma,akishindwa hapo anakata rufaa kwa Rais ambaye kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu utakua ni uamuzi wa mwisho yani FINAL.Akiwa hajaridhika hapo aende mahakama kuu na kufanya Judicial Review! Hamna kwenda CMA kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu,as long as huyo mtu ni mfanyakazi wa umma,yani Public servant!!

Excellent,

Tena huko Mahakamani atumie Rule 26 of the “Labour Court Rules, 2007 [GN. No. 106/2007]”.

Kumbe mpo watu wenye akili kwenye hili jukwaa.
 
Kwa hayo maelezo yako alitakiwa kwenda kukata rufaa kwa kamisheni ya utumishi wa umma,akishindwa hapo anakata rufaa kwa Rais ambaye kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu utakua ni uamuzi wa mwisho yani FINAL.Akiwa hajaridhika hapo aende mahakama kuu na kufanya Judicial Review! Hamna kwenda CMA kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu,as long as huyo mtu ni mfanyakazi wa umma,yani Public servant!!
Na hiyo rufaa ni ndani ya siku 45 tu akichelewa hapo ndio basi tena.
 
Back
Top Bottom