Habari Watanzania,
Katika miezi kadhaa sasa, kuna jambo limekuwa likijirudia sana.
Jambo hili ni ZITO sana na wala si la kuchukulia mzaha hata kidogo.
Jambo lenyewe ni hili:
Mfumo wa TRA, hasa TANCIS ambao ndio unaotumiwa na Idara ya Forodha (Customs) kukusanya Mapato ya bidhaa zinazoingizwa nchini, umekuwa ukifanya kazi either nusu, au kuzima kabisa kwa muda.
Mfano tangu jana tarehe 09/09/2022, saa tano (saa 5:00 usiku) usiku, mpaka sasa muda huu saa 12 jioni tarehe 10/09/2022, mfumo huo wa TANCIS umesimama kutoa Control Number za kulipia ushuru/maduhuri ya serikali.
Ifahamike kwamba kusimama kwa mfumo kutoa hizo Control Number, hakuna malipo yanayoweza kufanyika.
Nisingeandika jambo zito kama hili kama lingekuwa limejitokeza mara moja.
Wanaoweza kufuatilia zaidi, wajiridhishe.
Hii hutokea karibu kila wiki, inaweza kuwa siku moja, au masaa kadhaa ya siku flani.
Sisi wateja tunapata changamoto sana.
SWALI LA MSINGI NI HILI;
Je, wakati mfumo unasinzia kufanya kazi kitu flani, ni nini huwa kinaendelea huko ndani?
Je, baada ya mfumo kurejea, tuna uhakika gani kwamba malipo kadhaa hayajachezewa?
Na kwa nini itokee kila wiki, au mara mbili kwa mwezi? Ni kina nani wanufaika wa hili jambo zito hivi?!
Asante.