John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Je Mizimu Ipo au ni Maneno ya Watu
Mizimu ni Nini
Mizimu ni maroho wa kuzimu walio wakuu wa giza ambao wanajimilikisha familia, ukoo au eneo ili watu wa eneo hilo wawe chini ya utawala wao na maelekezo yao. Mizimu ni miungu inayowamiliki watu wa familia fulani, au ukoo fulani, au eneo fulani au jamii fulani.
Kwa Nini Mizimu Ndiyo MIUNGU
Hii ni kwa sababu mizimu humiliki nchi fulani tu, au ukoo fulani tu au eneo fulani tu. Kumbu 6:14 inasema “Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao”. Maana yake kila taifa lina miungu yake.
Taifa kibiblia ina maana jumuiya ya watu wenye historia moja na utamaduni mmoja. Hivyo, hata ukoo au kabila au nchi au watu wa eneo moja wanaweza wakawa na miungu yao.
Ndiyo maana ukisoma maandiko utaona mataifa wasiomcha Mungu walikuwa na miungu yao, kwa mfano miungu ya Waamori, miungu ya Wakaldayo, miungu ya Wamisri, nk
Mungu anatukataza kunyenyekea kwa mizimu wala kuitumikia mizimu. Mungu anataka tuangamize mizimu. Kutoka 23:24 “Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande”.
Mizimu ni watendakazi wa shetani, ili kuhakikisha wewe unayehusika unamilikiwa na shetani na kufanya mambo ya kishetani. Mungu hataki wateule wake wahusike na mizimu, yaani miungu.
Mfano ni kule Misri. Kulikuwa na mizimu ambayo ilikuwa inawamiliki Wamisri, lakini Mungu alipokuja kuadhibu Misri, aliadhibu hadi miungu ya Misri. Yaani, Mungu aliiadhibu hadi mizimu inayowamiliki Wamisri. Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana”.
Mizimu ni maroho wa kuzimu wanaomiliki jamii fulani, ukoo fulani au familia fulani na kushinikiza watu hao kufanya mambo ya kishetani au yanayompa shetani faida. Hujawahi kuona ukoo mzima ni walevi au watumia sigara na ugoro? Hujawahi kuona ukoo mzima ili uwe tajiri lazima utoe kafara mtoto wako au kafara ya mume au mke? Hujawahi kuona ukoo mzima ni wazinzi na waasherati? Wengine hujikuta katika maovu hayo kwa sababu wanamilikiwa na mizimu inayowaelekeza katika hayo, maana mizimu ni miungu yaani watenda kazi wa shetani.
Ni vigumu kumhubiria injili mtu aliyeshikiliwa vyema na mizimu/miungu. 2Wakorintho 4:3-4 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.
Watu wengine hata akiwa mtu wa kanisa, anakuwa mkristo baridi au vuguvugu, maana hajafunguliwa kwa maombi. Kuna mtu mwingine akishika Biblia tu kusoma, kichwa kinakuwa kizito na anasinzia hapo hapo, hata kama ni saa moja tu iliyopita ameamka kutoka usingizi wa usiku, lakini ukimpa gazeti au kitabu tamthilia, atasoma bila usingizi na anaweza kusoma kitabu kizima kwa saa tatu tu, lakini hawezi kusoma kurasa mbili za Biblia. Huko ni kumilikiwa na mizimu.
Mizimu Inavyoingia Kwenye Familia
Mizimu huingia katika familia kupitia kafara, matambiko, mazindiko, maagano ya kishetani au mikataba ya kishetani ya kiongozi wa familia na nguvu za giza. Kwa mfano: baba wa familia anaenda kwa mganga ili kuweka ulinzi wa kipepo kwake na kwa familia yake, na huko kwa mganga anatoa kafara, labda ya mbuzi. Kwenye ulimwengu wa roho wa giza, wanateua mkuu wa giza mmoja ambaye ndiye mzimu/miungu ili kutekeleza matakwa ya kipepo ya familia hiyo. Baada ya miaka mingi, baba huyo ataongezeka hadi kuwa ukoo, maana alizaa watoto na watoto wake wakazaa, na wajukuu wake wakazaa, na kadri miaka inavyokwenda wanajikuta wanakuwa ukoo mkubwa.
Au, kwa mfano: mama anapoamua kwenda kwa mganga wa kienyeji na kuingia mikataba ya kishetani ili apate watoto, ujue watoto wote watakaotokana na tumbo lake watakuwa wameingia kwenye utawala wa mizimu aliyoenda kuitafuta mwenyewe kwa mganga.
Dalili za Kumilikiwa na Mizimu
Ukiwa kwenye uwepo wa Mungu kisha unaona kero au unatamani uondoke eneo hilo
Mfano kanisa zima mko katika maombi na nguvu za Mungu zimeshuka lakini wewe hujisikii vizuri kuwepo hapo muda huo tu wa nguvu za Mungu kushuka, unatamni kwenda nje ya kanisa, yaani unaona kero kuwepo katika uwepo wa nguvu za Mungu.
Kila mara ukiwa kwenye ibada, unasinzia wakati tu wa Neno na maombi
Hakikisha unaombewa ili kuvunja muunganiko kati yako na maroho hao wa kuzimu.
Wewe binafsi au kundi kubwa la watu katika ukoo wenu au familia yenu mnateswa na tabia chafu za aina moja. Mfano kwenye ukoo wenu watu wengi ni watu wa pombe, wizi, uongo, ndoa za wake wengi, kuoa na kuacha, kuzalia nyumbani, ukahaba, sigara, uzinzi, n.k
Miguu kuuma kwa ndani au kuwa kama inawaka moto kwa ndani
Unakuta mtu ni mzima lakini kuna muda miguu yake inakuwa inauma na kuwa kama inawaka moto.
Kuota mara kwa mara Wanyama, hasa nyoka mkubwa au ng’ombe akikufukuza au akikulinda. Ukiona nyoka mara kwa mara akikufukuza maana yake huyo nyoka ni nguvu za giza, hasa majini au mizimu.
Kuota watu waliokufa wakikupa maelekezo ya kipepo
Hii ni niia nyingine ya mizimu kufanya kazi, hivyo vunja muunganiko kati yako na hizo nguvu za giza.
Ukianza kusoma Biblia kichwa chako kinakuwa kizito au wakati mwingine kichwa chako kinaanza kuuma au unapata usingizi ghafla ili tu usiendelee kutafakari Neno la Mungu.
Unapokuwa unaombewa unasikia kichwa chako ni kizito sana na unajisikia vibaya isivyo kawaida.
Namna ya Kujitenga na Mizimu ya Ukoo au Familia
Kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi wako, yaani kuokoka
Yohana 1:12-13 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”
Usifanye ibada ya kishetani ya namna yeyote ile.
Ikimbie ibada ya sanamu: 1Wakorintho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu”.
Usifanyie kazi maelekezo ya aina yeyote ya kishetani au ya mizimu
Mfano ni huyu alienda kuuliza kwa mizimu akaishia kufa, maana Mungu alimwadhibu kwa kosa hilo. 2Wafalme 1:3-4, 17 ″Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi sasa, Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka. ……. Basi mfalme Ahazia akafa, sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya. ……”
Haribu madhabahu za giza na choma moto vitu vyote ulivyonavyo vinavyotokana na mizimu ulivyopewa na waganga au ulivyoelekezwa na waganga. Kama huwezi, wapelekee watumishi wa Mungu watavichoma. Kutoka 34:13 “Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao”.
Fanya maombi
Mizimu au miungu huingia sehemu kwa uhalali kupitia kafara iliyotolewa, hivyo hata vita ya kuiondoa hiyo miungu siyo vita ndogo. Wakati mwingine inabidi kuomba maombi ya vita, ukishirikisha watumishi wa Mungu.
Kama nguvu yako ya maombi ni ndogo, tumia sadaka kwenye maombi yako, ili kutengeneza agano la Mungu (Zaburi 50:5). Agano na Mungu likisimama ujue maagano ya miungu/mizimu yanatoweka na wanakuwa hawana uhalali tena wa kumtesa mtu huyo.
Tumeona kuwa mizimu wapo, wala si maneno ya watu. Hakuna anayeweza kubisha kuwa mizimu hawapo. Hii ni kwa sababu Mungu mwenyewe, amesema wapo, kupitia maandiko mbalimbali katika Biblia. Kwa mfano, Kutoka 12:12, Kutoka 23:24, 2Wafalme 1:3-4, 17.
Baadhi ya watu hudhani mizimu ni jambo zuri tu, wakati haimpasi kamwe mteule wa Kristo hujihusisha na mizimu, maana mizimu ni watenda kazi wa shetani.
Mizimu ni nguvu za giza, ambao huweka watu mbali na Mungu. Ukishirikiana na mizimu, hakika wewe huitaki mbingu, maana mizimu chanzo chake ni kuzimu.