BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
...unawaruhusu kununua mabehewa ya mitumba? Kwani Watanzania hatustahili kusafiri kwa mabahewa mapya?
TRL yapata mabehewa mitumba
Evance Ng'ingo
Daily News; Sunday,September 14, 2008 @00:03
Mabehewa 23 ya abiria yaliyoagizwa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka India yamewasili nchini tayari kwa safari za Kigoma na Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Bandari ya Dar es Salaam wakati wa upakuaji wa mabehewa hayo, Ofisa Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez, alisema kuwa mpaka jana tayari mabehewa sita yalikuwa yamepakuliwa kutoka melini.
Mabehewa hayo yamewahi kutumika huko India. Maez alisema kuwa kila behewa lina uwezo wa kuhudumia abiria 48 ambapo wakati wa mchana behewa linaweza kutumiwa kwa kukaa kama daraja la tatu, na usiku hutumika kama vitanda vya kulalia.
Maez alisema kuwa mafundi wa Reli kutoka nchini India wanatarajia kuwasili nchini wiki ijayo kwa ajili ya kufanyia marekebisho mabehewa hayo kabla hayajaanza kazi mwezi ujao. Maez alisema kuwa mabehewa hayo yatasafirisha abiria zaidi ya 1,104 hivyo inatarajiwa yataboresha safari za kwenda na kutoka mikoa ambako TRL inatoa huduma. Maez alisema kuwa kama TRL ingeagiza mabehewa hayo kutoka viwandani ingechukua zaidi ya miaka miwili hivyo ingesababisha mtafaruku kwa watumiaji wa huduma hiyo ya treni.