Je, Mkuu wa Mkoa Katavi apiga marufuku Walimu wa kujitolea?

Je, Mkuu wa Mkoa Katavi apiga marufuku Walimu wa kujitolea?

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
863
Reaction score
1,534
Ikiwa serikali inasema kipaumbele kwenye ajira 6000 zilizotangazwa na Rais, Samia kuwa ni walimu waliojitolea, mkuu wa mkoa wa Katavi bw. Juma Homera, amewahi kupiga marufuku walimu hao kufundisha katika mkoa wake na kudai Serikali inaajiri walimu kila siku.

Msikilize kwenye video hapa chini.

Je, kama serikali itaendelea na msimamo wake wa kuajiri walimu waliojitolea haioni kwamba itakuwa haiwatendei haki walimu hawa walioonesha nia ya dhati ya kujitolea lakini wakakataliwa na mkuu wa mkoa na maeneo mengine???
 
Hujamuelewa mkuu wa mkoa, alichomanisha hapo, kuna walimu wengi wapo mjini hawataki kwenda vijijini, hivyo shule za vijijini kukosa walimu, na wananchi kutozwa hela kwa ajili ya kuwalipa walimu wa mikataba!!
 
Nadhani atakua ameongelea manispaa ambako mara nyingi kuna waalimu wa kutosha angalau.

Nikikumbuka miaka ile nasoma mwanzoni mwa miaka ya 2000 bila hawa waalimu hasa washkaji waliokua wamemaliza form six wakiwa wanasubiria kwenda chuo hasa waliokua wanatokea kule bush kwetu kweli kutoboa ingekua ngumu, ngumu sana.

Shule ilikua porini, mwalimu mmoja head master, baadae tukaletewa mwingine, walikua wanakuja wanaondoka. Bila hawa wa kujitolea, tena miaka ile wazazi walikua wanachanga elfu 3 tunawalipa hawa jamaa kwa mwezi, sidhani hata mishahara yao ilikua inafika 40,000 kwa mwezi ila walitufundisha kwa kujitoa, kwa moyo mmoja.

Nawakumbuka sana walimu wangu wa kujitolea, NM wasalimie Pennsylvania, D wagawie akili watoto huko Simiyu, DK tukagulie mashirika yetu na halmashauri zetu, wapige hati chafu wote😂. PK kamata hao wahalifu wote tupa ndani wanyime dhamana 😂.

Mimi binafsi na appreciate sana hawa waalimu, bila wao nisingefika hapa na hii kazi yangu ya kuokota makopo nisingekua naifanya, labda sasa ningekua Katoro nachimba dhahabu ama Mirerani nachimba Tanzanite ama kule Makongorosi Chunya, Lupa Tinga Tinga Nachimba dhahabu.

Watu wote ambao mmewahi kua waalimu ama wa kujitolea ama wa kuajiriwa rasmi, heshima kwenu wakuu.
 
Ikiwa serikali inasema kipaumbele kwenye ajira 6000 zilizotangazwa na Rais, Samia kuwa ni walimu waliojitolea, mkuu wa mkoa wa katavi bw. Juma Homera, amewahi kupiga marufuku walimu hao kufundisha katika mkoa wake na kudai serikali inaajiri walimu kila siku.

Msikilize kwenye video hapa chini
View attachment 1778201
Je, kama serikali itaendelea na msimamo wake wa kuajiri walimu waliojitolea haioni kwamba itakuwa haiwatendei haki walimu hawa walioonesha nia ya dhati ya kujitolea lakini wakakataliwa na mkuu wa mkoa na maeneo mengine???
Huyo naye tayari kashalewa madaraka
 
Ccm haijawahi kuwa na watumishi wenye weledi maana kila kitu kwao ni maigizo.
 
Hahaa mwanangu msovero inaonekana ww ni graduate ambaye hujakubali kua ajira ni janga ,mkuu tusiziwazie sana hizi ajira mkuu tukipata bas tusipopata basi, naona thread zako nyng znahusu ajira ajira
 
Back
Top Bottom