bily
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 8,029
- 5,796
Habari wanajamvi kuna kitu ambacho kamwe siwezi kulisahau hasa masuala ya migomo chuo kikuu cha Dsm (UDSM) nakumbuka sana pale wanafunzi walipokua wakipata hadha ya maji katika kampasi kuu (MAIN CAMPUS) huku wenzao wa kampasi ya mabibo wakichekelea nakumbuka kuna siku watu walianza kuamasishana na kuimba nyimbo kadhaa ndipo msafara ulipoelekea katika makazi ya makamu mkuu wa chuo VC MUKANDALA watu wakavunja geti ila vc hakuwepo ndipo watu wakaamua kwenda kuoga swimming pool bahati mbaya kiongozi wa HALL TWO akafariki dunia baada ya kuzama kwenye kina kirefu cha maji nakumbuka alikua Mwenyekiti wa HALL TWO.RIP haya na mengine ila pia nakumbuka wakuu wa kunji ambao walikua wanatikisa kama SILINDE, OWAWA, ODWANG-MGANDA. dah ilikua ni noma aise wengine wanaweza elezea zaidi
''UNIVERSITY IS A PLACE WHERE PEOPLE'S MINDS ARE TRAINED FOR CLEAR THINKING AND FOR INDEPENDENT THINKING'' Nyerere
''UNIVERSITY IS A PLACE WHERE PEOPLE'S MINDS ARE TRAINED FOR CLEAR THINKING AND FOR INDEPENDENT THINKING'' Nyerere