Kuna huyu mwalimu alikuwa anaitwa Mwang'onda, alikuwa balaa, alikuwa anachapa kama hana akili nzuri na jicho moja alikuwa chongo, basi siku moja majamaa wametoka darasani wameenda toilet kujificha, si akawaibukia, kipindi hiko shule ya sekondari haijawekewa uzio, basi majamaa walimzungusha choo kile kama mara ishirini, yaani ilikuwa patashika, wengine waje na vituko vya maticha wa kibasila wale waliosoma pale 1991 hadi 1997