Je, mpira wetu upo salama? Mwenye CV ya Almasi Kasongo

Je, mpira wetu upo salama? Mwenye CV ya Almasi Kasongo

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Jana nimemsikiliza huyu sijui ndio mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi alivyokuwa anaongelea msimu mpya wa Ligi kuu, ukweli nimepatwa na hofu sana.

Anasema wanaendelea kutafuta wadhamini zaidi ya Azam na zimebaki siku chache sana sasa sijui hao wadhamini kwanini hawakutafutwa mapema. Naomba mwenye CV ya huyu ndugu ili tujue mpira wetu upo salama ama.

FB_IMG_1632220986201.jpg
 
Wanaendelea Kutafuta Wadhamini zaidi Ya Azam....Tatizo Lipo wapi hapo ?
Utopolo huwa Wanalaumu kila Kitu...! na Wewe Uto?
Umejuaje kama alie uliza ni utopolo?

Soka letu ili liwe salama ni lazima liendeshe na watu wenye maarifa makubwa na wenye weledi mkubwa

Hakuna kipindi ambacho TFF ilikuwa salama sana kama kile Leodger chilla Tenga
 
katika vitu vinavyochangia kuzorotesha mpira wetu miongoni mwake ni bodi ya ligi...imejaa viazi mbatata tupu, watu wanawaza fine tu waneemeshe matumbo yao, siyo influential wala smart kuwa pale, ligi inaanza wiki ijayo, hii leo hata mdhamin hajulikan!

Azam wametoa pesa ya TV rights kwa awamu ya kwanza wao wanazipeleka kwenye semina na kozi za marefa ili tu wapate channels za kupiga...ovyo kabisa!
 
tatizo hawa watu hawapitii process za kawaida za kuchaguliwa au kushindanishwa, wanapeana kiundugu hawa ndio wanakagua viwanja michezo ikianza wanavifungia
Hawapelekwi kindugu Mkuu, most of them ni "KITENGO"

Kasongo Almas, Boniface Wambura(siku hizi yuko TFF) na wengine kibao wako hapo kutotana na ajira zao za kificho ma wala sio kwa sababu ya kuwa wanamichezo wazuri
 
Baada ya kubaki timu 16 ungetegemea ligi kuisha mpaka mwezi wa 5, sio wa 7 tena

Sitapinga kuleta wageni waendeshe mpira wetu as long as wanaleta weledi, ufanisi na uzoefu.

Kibongobongo tunapeana michongo kimazoea, hatuangalii competence & qualifications za watu.
 
katika vitu vinavyochangia kuzorotesha mpira wetu miongoni mwake ni bodi ya ligi...imejaa viazi mbatata tupu, watu wanawaza fine tu waneemeshe matumbo yao, siyo influential wala smart kuwa pale, ligi inaanza wiki ijayo, hii leo hata mdhamin hajulikan!

Azam wametoa pesa ya TV rights kwa awamu ya kwanza wao wanazipeleka kwenye semina na kozi za marefa ili tu wapate channels za kupiga...ovyo kabisa!
Kuna faini zinapigwa kihalali ,kuna timu zinaruka ukuta au kupitia milango isiyo rasmi hata zikipigwa faini wanarudi makusudi.

Faini zingine za bahati mbaya ni Kama ambulance kuchelewa uwanjani
 
Ulitaka wakununulie matikiti maji?
Mbona unataka kuwapangia matumizi ya pesa hizo?
katika vitu vinavyochangia kuzorotesha mpira wetu miongoni mwake ni bodi ya ligi...imejaa viazi mbatata tupu, watu wanawaza fine tu waneemeshe matumbo yao, siyo influential wala smart kuwa pale, ligi inaanza wiki ijayo, hii leo hata mdhamin hajulikan!

Azam wametoa pesa ya TV rights kwa awamu ya kwanza wao wanazipeleka kwenye semina na kozi za marefa ili tu wapate channels za kupiga...ovyo kabisa!
 
Hawapelekwi kindugu Mkuu, most of them ni "KITENGO"

Kasongo Almas, Boniface Wambura(siku hizi yuko TFF) na wengine kibao wako hapo kutotana na ajira zao za kificho ma wala sio kwa sababu ya kuwa wanamichezo wazuri
Unataka kuja na hadithi yako ya ajabu sana. Eti KITENGO huyu Wambura na Kassongo wawe KITENGO labda. Leta cv ya Kassongo.
 
Kiukweli wadau mmetoa maoni yenu kwa kadri ya upeo na uelewa wenu,kiufupi Almasi Kassongo ni msomi mbobevu amesoma Udsm kwa degree ya kwanza na akajiendeleza kwa Masters nchini Uingereza,katika medani ya mpira yeye ni mdau mkubwa kwani ameuishi mpira tokea akiwa shule ya msingi Ilala akiwa anacheza timu ya shule na pia timu ya mtaani iitwayo African stars chini ya mwalimu nguli marehemu Edwin Mloka maarufu kama Father.

Baadae akachezea Fc Boom ya Ilala Bungoni na pia Pentagon Hotspurs a.k.a Msimbazi Rovers ambayo imeshiriki hadi ligi kuu miaka ya mid 2010-2020,Almasi ana sifa stahiki za kuwa katika nafasi anayoishikilia na kabla ya kuwa hapo ameshakuwa mwenyekiti wa DRFA na yote yanayotokea hauwezi kumuweka kando iwe +ve au -ve na unapotaka kuinyooshea kidole taasisi ebu toa lawama kwa uwajibikaji wa jumla na si kumlaumu mtu binafsi ama uwe na tatizo nae binafsi kwani hadi hatua hii bodi ya ligi ni sehemu tu ya Tff na haijakuwa na mandate yakuweza kufanya majukumu yake moja kwa moja.

Hivi unawaacha wote ktk suala la udhamini unamuattack Almas personal kwanini? Je hata huo udhamini uliopo kutoka taasisi mbalimbali mbona hamumpi kongore zake na mnapeleka direct kwa tff?

Tuache majungu penye haki tuipe nafasi yake na penye udhaifu tukosoe kwa nia ya kujenga na si mashambulizi binafsi,ni wakati gani toka ligi ya bongo uijue timu zimekuwa na uhakika wa kupata pesa kam msimu huu? Kasongo anatosha sana
 
Umeona wapi duniani pesa za TV rights zikatumika kwenye semina za marefa!
hivi Tv rights ndani ya hzo pesa si kuna pesa ya uendeshaji kwa taasisi? Au ulijua za taasisi unanunulia tv? Huo mpira unaotarajia kuuona ikawa hao waamuzi wanaboronga je kesho utapata hamu ya kukaa kutizama tena?

Semina na kutoa awareness kwa watekeleza majukumu ni moja ya uhai wa taasisi au ulitaka kwakuwa wameshakuwa tu waamuzi basi haya nendeni
 
Back
Top Bottom