Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kauli ya msajili ya vyama vya siasa na Jeshi la polisi kuhusu BAVICHA ina kila dalili kwamba watu hawa wamekaa kikao cha pamoja na kutoka na maazimio.
Kwa mtizamo wangu inaleta picha kwamba UVCCM wameshindwa kuandaa wanasiasa. Tumeona Zanzibar kwamba ilibidi Rais awepo ndipo agenda zao ziweze kusikika.
Wenzao wanapoandaa jambo lao ni vyema wakajifunza namna yakupambana nao kisiasa
Hata sisi wana CCM tumefika mahali sasa huku mitaani tunaonekana kama hatuwezi kuzaa au kuwa na jamii yenye akili na uwezo wakujipigania.
Kila siku sisi wana CCM ni watu wakusaidiwa kuendesha siasa. Kwanini tusiachwe tupambane nao? Kwanini tuamini viongozi wa kitaifa pekee ndio wanaweza kukijenga chama?
Leo bila nchimbi hatufanyi siasa, hata mawaziri wamekosa nguvu kwa sababu wanapokuja kufanya kazi wananchi na wana CCM tumeshindwa kuamini kwamba hawa ni wenzetu tuwaunge mkono.
Wana CCM tumekuwa wa kwanza kushangilia wenzetu waliotumbuliwa, tumekuwa wa kwanza kubaguana kwa uwezo wetu wa kiuchumi na familia tunazotoka
Haya yote yanatokana na wana CCM kuwaachia vijana wa upinzani wafanye siasa na kuonyesha talenti zao lakini wakwetu wakiwa bubu.
CCM siyo chama cahukuwekeza kununua wanasiasa kutoka chadema. Kila siku tunataka kununua wanachama wa chadema, wakigoma ndio unasikia wamenyimwa kuandamana na kufanya siasa
Yaonekana CCM walipanga mkutano wa chadema usifanyike na wakitegemea akina Lisu wafarakane. Leo tumeambilia msigwa ambaye hana hoja badala yake anaendelea kuifanya CCM ionekana watu wake wanawaza chadema kuliko wanavyoweza kuwaza matatizo ya wananchi.
Niliposikia Nchimbi anamkaribisha Lisu CCM ndipo nilipo kubali kwamba CCM tumekosa viongozi tunatafuta viongozi.
Mwisho, CCM tuacheni siasa za kumtegemea msajili na polisi. Jinsi polisi wanavyopiga story na vijana wa chadema hapa Iringa unatambua kabisa hata wao polisi wanatuchukia sema wanafanya unafiki.
Hakuna polisi anaweza kucheka na adui, wanatambua kwamba hapa CCM imekwama na imekosa hoja. Tunataka tufanye siasa wenyewe bila upinzani?
Pia soma:Kuelekea 2025 - Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani