Je, mstaafu akifariki pensheni anaendelea kupewa mwenza wake au nayo inakoma?

DAVID PALMER

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2020
Posts
318
Reaction score
1,597
Habari zenu bhana

Naomba niende moja kwa moja najua ntapata wajuzi wa kunishauri.

Baba yangu alikua mwalimu kabla hajastaafu. So alikua anapokea penshen ile ya kila mwezi mpaka alipofariki mwaka juzi 2021. Alifariki akiwa na miaka 74.

Ile penshen iliingia kwa miezi mitatu tuu then ikakoma. Na ndo ilikua inamsaidia mama yetu pale nyumban. Ilivokoma tukajua labda mstaafu akifariki na penshen inakoma.

Mama yetu ni mjane na ana miaka 71 sasa. Sasa kuna kila dalili kuwa zile pesa bado zinalipwa ila zinaenda kwenye mifuko ya watu wengine. Nimehisi hivo maana bima ya mama bado inafanya kazi. Na kuna connection kati ya bima na ile pension. Kama pension isingekua inaingia bima pia ingefika ukomo wake. Mama yeye ni mkulima tuu hajawahi ajiriwa popote. Yuko njombe vijijini na mimi niko Dar.

Nikafatilia nyuzi za humu JF nkaona kumbe mstaafu akifariki basi mjane anaendelea kupokea ile pension ya kila mwezi mpaka nae akifariki au kuolewa.

So naomben mnisaidie ktk hili. Jee ni kweli mama anastahili kupokea pension kila mwezi? Kama ni kweli basi nitumie njia gani kurudisha haki hii.

Natanguliza shukran.
 
Pensheni ya kila mwezi ni kwa ajili mstaafu tu na uwa wanafanya uhakiki kila baada ya miezi 6 mstaafu asipoenda kuhakikiwa wanasimamisha pensheni wanachukulia uenda tayari amekufa kuhusu bima sina uhakika sana ila nasikia muhusika ambaye alikuwa mtumishi akifariki wategemezi wake wataendelea kupata huduma kwa miaka mitatu baada ya hapo huduma inasitishwa.
 
Pension inakoma ila bima ya mke/mume inaendelea hadi nae atakapoitwa kwa muumba wake. Hii bima pindi unapostaafu kadi zote zinarudishwa isipokuwa ya mwenza. Hivyo hakuna makato ya kupeleka bima. Kwa maneno mengine pension na bima hazitegemeani. Asante
 
Pension ni kwa mstaafu tu ambaye naye huhakikiwa mpaka na vidole kila baada ya mwaka mmoja.

Ukifariki watu wasipotoa taarifa ya kifo hasa mwajiri utaingiziwa hela mpaka ifike tarehe ile ya kuhakikiwa ndipo hela itakoma.

Mama yako hana hiyo sifa ya kuingiziwa pesa.

Kuhusu bima ni kama nayo ina expire date, ambapo mwajiriwa ataenda ku renew, na ujue bima ya afya baada ya kustaafu ni wewe na mwenza tu, so tegemea pia mama kusitishiwa bima muda wowote.

Serikali inatupenda tunapoitumikia tukiwa na nguvu, baada ya hapo serikali haina taimu na wewe.

Jiweke sawa kumtunza mama yako mzazi.
 
Ccm ndio walileta huu wizi, pumbavu Sana!
 
CCM inaingiaje hapa...?
Wapitisha sheria za Kijinga fikiria mbunge anaejua kusoma na kuandika tu analipwa pensheni kubwa akimaliza miaka yake 5 ya ubunge ili hali hakuchangia hata shilingi tano na bado analipwa mshahara na posho bila kukatwa hata kodi! Mwalimu alieteseka na vumbi la chaki kwa miaka 30 anapewa pensheni yake aliyokatwa kiduchu tu kwa kikotoo kipya huku akifa na miaka 61 habari yake imeishia hapo na ela yote inaishia kwenye miradi hewa ya wajanja wa CCM.
 
Jaman naomba msaada wenu ukimaliza taratibu zote za mirathi fedha hutoka ndani ya miezi mingapi???
 
Jaman naomba msaada wenu ukimaliza taratibu zote za mirathi fedha hutoka ndani ya miezi mingapi??
 
Habari zenu bhana

Naomba niende moja kwa moja najua ntapata wajuzi wa kunishauri.

Baba yangu alikua mwalimu kabla hajastaafu. So alikua anapokea penshen ile ya kila mwezi mpaka alipofariki mwaka juzi 2021. Alifariki akiwa na miaka 74.

Ile penshen iliingia kwa miezi mitatu tuu then ikakoma. Na ndo ilikua inamsaidia mama yetu pale nyumban. Ilivokoma tukajua labda mstaafu akifariki na penshen inakoma.

Mama yetu ni mjane na ana miaka 71 sasa. Sasa kuna kila dalili kuwa zile pesa bado zinalipwa ila zinaenda kwenye mifuko ya watu wengine. Nimehisi hivo maana bima ya mama bado inafanya kazi. Na kuna connection kati ya bima na ile pension. Kama pension isingekua inaingia bima pia ingefika ukomo wake. Mama yeye ni mkulima tuu hajawahi ajiriwa popote. Yuko njombe vijijini na mimi niko Dar.

Nikafatilia nyuzi za humu JF nkaona kumbe mstaafu akifariki basi mjane anaendelea kupokea ile pension ya kila mwezi mpaka nae akifariki au kuolewa.

So naomben mnisaidie ktk hili. Jee ni kweli mama anastahili kupokea pension kila mwezi? Kama ni kweli basi nitumie njia gani kurudisha haki hii.

Natanguliza shukran.
Kama mlitoa taarifa hazina, basi ni miezi 3 ndio mane atalipwa kama ulivyoeleza.
 
Kama cjakosea nilisikia hutolewa kwa mjane kwa mwak mmoja kam si mitano endapo mume wake wa ndoa amefark
 
Back
Top Bottom