Je mtandao wa X (twitter) umezimwa Tanzania?

Je mtandao wa X (twitter) umezimwa Tanzania?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Mtandao namba 1 kwa kuibua mijadala mbalimbali ulimwenguni maarufu kama X zamani ukijulikana kama Twitter ni kama umezimwa nchini Tanzania. Ukijaribu kuingia kwa njia ya kawaida unagoma mpaka utafute VPN.

Je ni tatizo la kimtandao au ndio umezimwa kimyakimya?
 
Je ni tatizo la kimtandao au ndio umezimwa kimyakimya?
Nafikiri ni mtandao tu, kuna wakati inakubali na kuna wakati inagoma.

BUT kwa nchi yetu na tabia za watawala tulionao, KUZIMWA ni jambo linalowezekana kabisa. Maana harakati za kueleza ukweli na kuwafumbua watanzania zimejaa huko.

Kwa Tanzania, siku zote kutafuta ukweli ni sawa na kumenya kitunguu, kila ganda utalofunua lazima likutoe machozi.

Failed State.
 
Sakata la majizi ya CCM kufanya ubadhilifu wa fedha za umma kwa kupitisha ile kauli ya mama yao kuwa wataanza kununua umeme nnje, wakati huo hapa nchini mabilioni ya pesa yameshatumika kujenga bwawa ambalo walisema wenyewe litaweza kuzalisha umeme mwingi na bei za umeme zitashuka, huku changamoto ya mgao ikiisha, maajabu ni kwamba wameshasahau kauli zao wanakwenda kupoteza mabilioni mengine kufuja katika manunuzi yasiyoeleweka.

Kwa ushenzi huu ili kuwapoteza raia wasihoji wala kufanya mijadala hawa majizi naona wakalegeza eneo(X) ambalo ndiko kuna mlipuko wa hoja nyingi za kisiasa dhidi yao
 
Kwa Upepo ulivyo uchaguzi mkuu mitandao tote ya kijamii itazimwa. CCM Must Go!!
 
Back
Top Bottom