Kwanza elimu ya bongo kuanzia chekechea mpaka chuo imechakuliwa mno....yani ipo hovyo-hovyo sana.
Waziri wa elimu ana uwezo wa kulala na mke wake, wakamwangalia mtoto wao wa kike au wakiume na kuona hapendi mpira(ye na game game na yeye), basi akaja na kutangaza michezo hamna. Toto likiwa kilaza kesho utasikia, hesabu zifutwe mashuleni.
Just angalia mitaala inavyochange kila uchao, serikali kwa sasa haina hela, wakasema mitihani ya darasa la 4 na form 2 waafute, baadae walivyoona wameikwaa wameirudisha tena wakati serikali ipo hali mbaya. Vipi ulishagundua mitihani ya form 4 mwaka huu imefanyika ndani ya wiki 1 tu. 7 days equivalent to 4 yrs!! Ilimradi wanafunzi wakakae nyumbani kwani serikali haina hela ya kuwalipa walimu wasimamizi.
Elimu uchwara inayotolewa tanzania kwa sasa haina future, most of us tunategemea kuajiriwa, idadi inatisha ya jobless people huku kitaa, waliopo makazini zaidi ya 50% wana vyeti bandia, uswahili mwingi kwenye taasisi, elimu duni...yaani mambo mengimengi tu.