SoC04 Je, mtoto ni mali ya nani?

SoC04 Je, mtoto ni mali ya nani?

Tanzania Tuitakayo competition threads

Baba chenrich

New Member
Joined
May 5, 2024
Posts
3
Reaction score
3
TANZANIA TUITAKAYO

Je mtoto akizaliwa ni Mali ya nani ? “

Screenshot_20240512-202634_1.jpg

Chanzo : successwisdom​

UTANGULIZI
Jamii na ulimwengu hujengwa na watu wenye afya bora na huzungukwa na watu halisi katika jamii yao, Nchi na ulimwengu utafanya mapinduzi makubwa sana pale tu ikianza kumjali mtoto toka kipindi Cha ujauzito wa mama.
Marifa mapana na ubunifu utaanzia mazingira haya na kuleta vizazi vilivyo na afya njema pamoja na maadili yaliyo tele kabsa, hii ndiyo “TANZANIA TUITAKAYO“

Tukitafakari yote tujue ya kwamba mtoto ana haki ya kua na afya bora na kujivunia kua yeye ni Mtanzania halali kwa uwajibikaji wa wazazi na jamii inayo mzunguka Kila siku. Hapo chini ni maboresho yanayo hitajika kumfanya mtoto mali halali ya jamii na kujiamini ya kwamba yeye ni bora na ni Mtanzania kweli.

Mtoto ndiye mama yetu, baba yetu, kiongozi wetu, hivyo uimala wake kiafya hutia amani na nguvu kubwa katika kupambania maisha yetu ya kila siku. Katika kuzingatia afya yake huanza pale tu pindi mama mjamzito akianza kujisikia dalili zake tumboni. Kwa kuboresha afya ya mtoto na ubora wake kua Mtanzania halisi serikali iweze kuboresha yafuatayo katika vituo vya afya Nchini;

Kua na Sheria ya mama mjamzito kufika mapema kituo Cha afya kabla ya kujifungua
Mafanikio ya mama mjamzito kuwasili mapema kituo Cha afya hujenga imani chanya Kwa wazazi wa mtoto kwani manesi watakua sambamba na mama huyo wakati wa mabadiliko yoyote anavyo jihisi wakati huo wa kujifungua.

Katika kuwasili mapema serikali iweke mda maalumu kwa mfano, mama mjamzito kuwasili kituo cha afya ndani ya siku Saba (7) kabla hajajifungua Kwa uangalizi maalumu wa madakitari. Kwa kuzingatia Sheria hii jamii itapata nguvu kazi safi na yenye afya iliyo tele kabsa Kwa kupambania nchi na mafanikio makubwa sana. Kwa kufanikisha jambo hili inamtaka mama mjamzito awe tayari kufanya hivyo kwa maisha ya mwanae kwa maana ya kuwahi mapema kituo cha afya, lakini pia serikali iweke mkazo mkubwa kwa atakaye shindwa kutekeleza Sheria hiyo itakayowekwa.

Kua na ofisi ndogo ya RITA katika vyituo vya afya
Ili kupunguza uzembe wa wazazi kufatilia vyeti vya kuzaliwa vya watoto mkoani au wilayani alipo zaliwa mtoto serikali iwezeshe upatikanaji wa ofisi ndogo ya RITA kitengo cha USAJILI VIZAZI NA VIFO ilikutoa vyeti vya vizazi katika vituo vya afya kwani kituo hicho kitachukua taarifa za mtoto moja kwa moja kutoka kituoni hapo mtoto alipozaliwa na kuzipeleka makao makuu ya RITA mkoani au wilayani ili mzazi aweze kupata cheti cha mtoto cha kuzaliwa hospitali apo na kuepusha msongamano wa watu mkoani wakifatilia vyeti vya kuzaliwa pamoja na Kadi ya kitambulisho Cha Taifa NIDA).

Kuongeza uhuru wa habari katika vituo vya afya
Uhuru wa habari katika vituo vya afya ni njian moja kubwa ya kutatua na kupunguza rushwa katika vituo vya afya kwani jamii itakua huru na kudhibitisha swala la rushwa na hongo katika maeneo mbalimbali ya vituo vya afya na hospitali pale tu ambapo mwananchi akiona dalili za hali hiyo.

Katika mazingira hayo ya rushwa ndipo madhara ya mama mjamzito anaweza kushidwa kujifungua kwa haraka na kumpumzisha mtoto aliyeko tumboni, kwamfano mazingira ya rushwa na hongo katika vituo vya afya na hospitali yanaweza kujionyesha wakati wa kupatiwa huduma kwa mama mjamzito pale tu atashindwa kuitwa jina lake ili apatiwe huduma na kuitwa mtu mwingine aidha alikuja nyuma yake kwa aliyetangulia. Kwa kitendo hicho mama mjamzito anaweza kushidwa kujifungua haraka na kupelekea kifo kwa mtoto, Kwa namna hiyo basi serikali iongeze Uhuru wa habari katika vituo vya afya ili kupunguza rushwa na hongo.

Kua na machine za kisasa za kujihudumia (Electronic Machine)
Kutokana na mapinduzi makubwa ya kitekinolojia serikali iwezeshe uwepo wa mashine za kisasa za kujihudumia na kazi yake iwe ya kutoa kadi yenye namba ya huduma ambayo mzazi mjamzito akifika kupatiwa huduma aweze kuchukua kadi hiyo ambayo itaonyesha kua yeye ni namba flani kupatiwa huduma na kwa kufanya hivyo utoaji wa huduma kwa mama mjamzito itapungaza changamoto zinazoendelea kuwakumba mama hao wajawazito ambayo ingesababisha ata kifo kwa mtoto kutokana na kuchelewa kupewa huduma.

Mwisho
Mapinduzi na mabadiliko huanza kwa maandalizi yaliyo ya awali kabisa kwa kuanza na watoto ambao ndiyo kizazi kinachoandaliwa kuleta mapinduzi na mabadiliko hayo ya kujenga Nchi iliyo bora na yenye mafanikio makubwa katika Karne. Hivyo ilikufanya hayo yote yatupaswa basi jamii na serikali kwa pamoja tuweze kuwajibika katika kutimiza ndoto za vizazi vijanvyo na jamii pia kuweza kujivunia mafanikio hayo yenye mabadiliko yatakayo letwa katika kipindi hicho Cha kizazi cha mafanikio na hii ndiyo #TANZANIA TUITAKAYO.
 
Upvote 1
Katika kuwasili mapema serikali iweke mda maalumu kwa mfano, mama mjamzito kuwasili kituo cha afya ndani ya siku Saba ( 7 ) kabla hajajifungua Kwa uangalizi maalumu wa madakitari
Pagumu hapo, maana mahesabu ya mimba na ujauzito au kibaiolojia tu huwa ni makadirio na matarajio 'at best'.

Badala ya kuwajaza wamama mahospitalini kitu ambacho sio kizuri kiafya, bora wabakie majumbani kwao watakujaga wakiwa kweli wanaumwa uchungu. Uhakika wa usafiri na ufikikaji uwepo.

serikali iwezeshe upatikanaji wa ofisi ndogo ya RITA kitengo cha USAJILI VIZAZI NA VIFO ilikutoa vyeti vya vizazi katika vituo vya afya kwani kituo hicho kitachukua taarifa za mtoto moja kwa moja kutoka kituoni hapo mt
Hili sawa sawia, mambo yote yawe mojakwamoja bila mlolongo mrefu maana mtoto kazaliwa na uthibitisho upo hapohapo
 
Pagumu hapo, maana mahesabu ya mimba na ujauzito au kibaiolojia tu huwa ni makadirio na matarajio 'at best'.

Badala ya kuwajaza wamama mahospitalini kitu ambacho sio kizuri kiafya, bora wabakie majumbani kwao watakujaga wakiwa kweli wanaumwa uchungu. Uhakika wa usafiri na ufikikaji uwepo.


Hili sawa sawia, mambo yote yawe mojakwamoja bila mlolongo mrefu maana mtoto kazaliwa na uthibitisho upo hapohapo
Jambo jema ndugu maana taarifa zinakuwepo sasa ni USUMBUFU kutoka hospital afu uanze kufatilia mkoani
 
Back
Top Bottom