Eti wakuu hii kitu inakuwaje au ndo hainaga formula maalum?
Habari!
Mazoezi yanaweza kukupa faida au hasara kulingana na utekelezaji wake ili kukukiga na suala husika.
Faida/kuzuia stroke (kiharusi) hutokana na kubadili/modify risks za stroke kama unene/uzito mkubwa, mafuta, kisukari nk.
Swali lako halina jibu la moja kwa moja. Hii inatokana na swali ulilouliza hutegemea vipengele vingine kama:
A: MAZOEZI
1: Aina ya mazoezi (inashauriwa yawe ni aerobics, yanayohusisha viungo vyote vya mwili kama kutembea kwa kasi nk.).
2: Kiasi cha mazoezi(yawe ni ya kiasi ambacho mwili wako unaweza kuhimili bila shida kwa kuzingati: matatizo mengine ya kiafya yaliyopo, umri, uzito nk.)
3: Mazoezi kupita kiasi huweza kuwa chanzo cha stroke na shambulio la moyo pia kuleta athari kwenye figo.(stroke/kiharusi: kwa wenye matatizo ya mapigo ya moyo/arrhythmias, wenye matatizo ya kuta za mishipa ya damu/anyurizimu nk.).
B: MWENENDO WA MAISHA
Mazoezi ni muhimu kuambatana na mabadiliko kwenye maisha.
1: Kunywa pombe kwa wastani
2: Kuacha kuvuta sigara
3: Kula chakula kwa kuzingatia mahitaji ya mwili, kazi au umri.
4: Kutumia dawa kwa usahihi hasa wale wenye matatizo ya kiafya kama: presha, sukari na matatizo ya mafuta/cholesterol.
Pia dawa ya kulainisha damu inapobidi.
5: Kutimia kwa wastani vinywaji vinavyopeleka moyo mbio kama: kahawa nk.