Je, Muokoaji Shujaa asingekuwa na Jina la 'Majaliwa' angesifiwa na hata Ushawishi wa Kumtunza 'Mifedha' ungekuwepo?

Je, Muokoaji Shujaa asingekuwa na Jina la 'Majaliwa' angesifiwa na hata Ushawishi wa Kumtunza 'Mifedha' ungekuwepo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Haya haya Waokoaji wa Ajali za baadae hakikisheni nanyi Majina yenu yawe yanafanana na ya Viongozi Wakuu na Waandamizi wa Serikali hii ya Awamu ya sasa ili yakitajwa tu basi wenye hayo Majina ( Wajina zenu ) waweze Kufurahi na kupata hata Ushawishi wa Kuwalazimisha Wakuu wa Mikoa mpewe Zawadi na muimbwe sana katika Media na Social Media mbalimbali sawa?

Na usitegemee kusikia Ajali ya Meli imetokea halafu Shujaa wa Kuokoa Watu akawa ni GENTAMYCINE Mwenye majina halisi ya NIDA na RITA hadi Pasipoti ya UHAMIAJI ya Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura kisha ukasikia Nasifiwa na kutakiwa kupewa Zawadi kwani Majina yangu yote haya tajwa hapa hayafanani na Kiongozi yoyote wa Serikalini hivyo nitaishia tu Kupongezwa ( Kukongolewa ) kwa maneno matupu na kuendelea kuyaishi haya haya Maisha yangu ya Umasikini ulionitukuka hadi katika Kope zangu za Macho.

Cc: adriz, Glenn, Daudi Mchambuzi, Bila bila, Sky Eclat, Bujibuji Simba Nyamaume, Slim5 etc.
 
Bila kumtaja big boss wako Matola uzi huu ni batili😂😂😂
Ninamkubali sana Matola anavyokupa za uso kwani wewe kwa Matola uko sawa na mandonga😅😅
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Ni muda wa Bibi kuiacha nchi na kwenda kuota moto imemshindaa(nje ya mada)
 
Zawadi ya shujaa inakutoa ukamasi sana, unateseka mno.
 
Ungekuwepo maana hilo jina la Jasiri ndio lililo mpa hiyo bahati walahi
 
Back
Top Bottom