Je mwaka 2011 ulikuaje kwako katika mahusiano?

CHIPANJE

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2011
Posts
321
Reaction score
53
Binafsi,hali haikua nzuri hata kidogo zaid i miez ya Feb na June.

Msichana ambaye tulikubaliana alipoamua kunisaliti na kuolewa na mwanaume mwingine kipindi cha mwezi wa kumi na moja ndipo alipofungua ndoa.

Kilikua ni kipindi na mwaka mgumu sana kwangu kwani nilifedheheshwa sana na hata baadhi ya mambo hayakwenda vizuri.

Kuhusu uzuri wa mwaka huohuo,ilipofika July nikampata msichana ambaye hadi hivi sasa ameonekana kua mwaminifu kwangu na kuniondolea wakati mgumu ambao nilikumbwa nao.Tukimaliza masomo tutapanga utambulisho rasmi kwa wazazi.

Je mwenzangu kwako ulikuaje?
 
Kila kitu kinatokea kwa sababu Mkuu....
Ukilijua hilo kila nyakati kwako utazitafsiri kwa furaha tu!

Chukua jukumu lako vilivyo kwa hicho kifaa chetu kipya kisikuponyoke....
Ah nimesahau kuhusu mimi na mapenzi yangu lol yalikuwa matamu sana....

Hebu cheki stori hii ya MALAIKA WANGU
 
kk soma utaliwa kichwa coz inaonekana ww bend 1, huwez fanya mambo meng kwa wakat m1, hata huyo she ulienae ukiliwa kichwa wajanja 2namchukua
 

hahahah...... Happy New Year to You & ur Angel!!! Usiwe unapotea sana basi mkuu.....
 
Mkuu unajuaje kuwa huyo uliyempata ni mwaminifu? Miezi mitano ni muda mfupi sana kuingia ktk mahusiano na kujipa matumaini kuwa umepata mke mwema! Ikumbukwe kuwa wewe ni kama nyati aliyejeruhiwa, ukimpata demu ambaye hajatulia na ikawa amepata story yako ya kupigwa chini, hapo ndipo utaona sarakasi za ajabu. Motive ya kuleta thread hii hapa, I guess ni huyo demu uliyempata, so think twice before you jump!
 
hahahah...... Happy New Year to You & ur Angel!!! Usiwe unapotea sana basi mkuu.....

Poa sipotei tena Mkuu wangu...
Heri ya niuu iya kwako pia..
Malaika yupo poa sana alitaka kukesha na mimi hapa jamvini ila kachemka, nishamlaza!

 

"Mpaka sasa ameonekana ni mwaminifu" hayo ndio maneno ya mtoa mada. Acha kumwekea vikwazo kwa lazima!!

@Mtoa mada. . . Pole na hongera.Usitishwe na mtu, kama mwenzio anaonekana ametulia endelea nae taratibu huku ukiomba awe ametulia kweli. Hauna haja ya kuanza kuwa na wasiwasi wakati mhusika hajakupa sababu.
 
Poa sipotei tena Mkuu wangu...
Heri ya niuu iya kwako pia..
Malaika yupo poa sana alitaka kukesha na mimi hapa jamvini ila kachemka, nishamlaza!


dah......inaonekana ye hakuwa na usongo na nyu mwaka, mi nilivokuwa nausubiri kwa hamu aisee sijui ka nitalala kabisa! Hapa natamani ingekuwa Idd ili nipige na ngoma za daku kwa msisitizo lol!!! Heheh hako kamalaika kako ukikasogelea tu we kambie mimi Kipipi nakatakia new year yenye heri, kazidi kukukamatilia zaidi hata usifurukute!!!
 
Poa sipotei tena Mkuu wangu...
Heri ya niuu iya kwako pia..
Malaika yupo poa sana alitaka kukesha na mimi hapa jamvini ila kachemka, nishamlaza!

So sweeet.

Happy new year jG!!
Naomba 2012 ukuwie mwaka mzuri wewe na Malaika. . . muwe na furaha pia amani tele.Mafanikio ndio kabisaaa mpaka mchoke wenyewe.Mbarikiwe sana!!
 
ebwana mi nilimpata msichana niliyekuwa kwenye mchakato naye kwa miaka miwili nikiendelea kumfukuzia. Hatimaye akanielewa na ameshafahamika kwa dada zangu coz ndiye mpango mzima.
 
So sweeet.

Happy new year jG!!
Naomba 2012 ukuwie mwaka mzuri wewe na Malaika. . . muwe na furaha pia amani tele.Mafanikio ndio kabisaaa mpaka mchoke wenyewe.Mbarikiwe sana!!

mmmhhhh... kweli mwaka mpya
 
Wewe na huyo new Gf wako Mjitahidi kufamiana likes na dislikes zenu itasaidia sana katika swala la amani.

Hap nu yr!
 
ebwana mi nilimpata msichana niliyekuwa kwenye mchakato naye kwa miaka miwili nikiendelea kumfukuzia. Hatimaye akanielewa na ameshafahamika kwa dada zangu coz ndiye mpango mzima.

Hongera brother!
 

Mkuu naona unafuata nyayo za Madam Ritta wa BSS, yeye kila kitu atakusifia tu hata kama tatizo lipo. Anyway, ni mtizamo tu.
 
Nilipigwa kibuti kitakatifu ingawa hakikunipunguzia lolote,otherwise ulikua mwaka mzuri sana kwangu financially,academically etc.over
 
Huo mwaka na uende zake. Niliona unachelewa sana. Ni mwaka uliokuwa mgumu sana toka tarehe moja, nilikuwa pembeni mwa kitanda alicholazwa mpenzi wangu pale Burhani hosptal. Siku kumi na nane baadaye alifariki pale muhimbili, sewahaji namba kumi.

Siutaki ule mwaka, heri umeenda.
 

pole mkuu, Mungu atakupatia mwingine. Namba kumi ipo kibasila siyo sewahaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…