Al maktoum
JF-Expert Member
- Nov 23, 2022
- 499
- 678
Wakubwa shikamoni , wadogo marahaba.
Siku moja miaka 21 iliyopita asubuhi nikiwa nimepumzika chini ya mti uliokuwa jirani na msikiti mmoja Moshi mjini baada ya kupata kahawa ya asubuhi, nilifuatwa na jamaa mmoja aliyenitaka nifanye JARIBIO LA KISAYANSI KUTHIBITISHA KUWA MUNGU YUPO!!
Kiuhakika nilitahayari sana na kubaki namshangaa huyo jamaa na hoja yake. Na hiyo ni kutokana na uchache wa elimu ya dini yakiislamu, na lugha ya kiarabu na hata lugha ya kiswahili (FASIHI) (Literature kiingereza) na adabu
(kiarabu الأدب العربي) niliokuwa nao kipindi hicho.
Yule jamaa baada ya kuona kwamba sina mpango wa kuifanyia kazi hoja yake akaanza kunihubiria kuwa yeye hazikubali dini zilizoletwa na waarabu na wazungu na kwamba yeye ni muumini wa dini za kibantu (bantuism) ambazo ndizo dini zilizokuwepo enzi za mababu zetu kabla hatujapokea dini za kigeni.
Mshamgao niliokuwa nao ulinifanya hadi nikasahau kumuuliza kama je, alishafanya JARIBIO LA KISAYANSI KUTHIBITISHA UWEPO WA MIZIMU ILIYOABUDIWA NA MABABU ZETU???!!.
Siku zikaenda na miaka ikapita . Siku moja nikiwa Tanga mjini rafiki yangu mmoja toka Unguja Zanzibar akanisimulia KISA CHA MWALIMU ALIYEKOSA AKILI.!!! Kisa hiki kilitokea katika moja ya nchi za kiarabu.
Mwalimu huyu ambaye alikuwa Zindiyqi ( mzandiki kd, ni mtu aliyeingia katika dini ya kiislamu akaisoma kwa nia mbaya ya kuivuruga, kuiharibu na kupotosha mafundisho yake matukufu.) siku moja aliingia darasani na kuanza kuuliza maswali kama ifuatavyo.
Mwalimu: Hal shuftum shajara?
(je mlishawahi kuona mti?)
Wanafunzi : ee na'am!. ( Ndiyooo!)
Mwalimu: Idhan, Al shajaratu mawjuuda ( kwahiyo mti upo)
Wanafunzi : ee na'am ( ndiyooo!)
Mwalimu: Hal shuftum bahran? ( Je mlishaona bahari?)
Wanafunzi : Ee na'am ( ndiyoo).
Mwalimu: Idhan, Al bahru mawjuud. ( Kwahiyo bahari ipo)
Wanafunzi : Ee na'am ( Ndiyooo!)
Mwalimu: Hal, shuftum sayyaara ? (Je, mlishaona gari?)
Wanafunzi : Ee na'am ( ndiyooo!!)
Mwalimu: Idhan , Assayyaaratu mawjuuda ( Kwahiyo gari lipo!)
Wanafunzi: Ee, na'am ( Ndiyooo!)
Mwalimu: Hal, shuftum Qitwaara?
( Je mlishaona gari Moshi?)
Wanafunzi : Ee na'am ( Ndiyoo!)
Mwalimu : Idhan Alqitwaaru mawjuudun . ( Kwahiyo garimoshi lipo!)
Wanafunzi : Ee na'am ( Ndiyooo!)
Mwalimu: Hal, shuftum Allaah?
( Je, mlishamuona Allaah?)
Wanafunzi: Laaa! ( Hapana! )
Mwalimu: Idhan, Allaah ghayru mawjuudun. ( Kwahiyo Allaah hayupo!)
Wanafunzi: !!!??? !!!??? '!!!???.
Mara mwanafunzi mmoja akanyoosha mkono.
Mwalimu: Enta bitaul Ee?? ( Lahaja ya kiarabu cha kienyeji عامية nchini Misri = (Wewe unasemaje?!)
Mwanafunzi : E'ndy suaal yaa ustaadh! ( Mwalimu naomba kuuliza swali!)
Mwalimu : Tifadh'al sal! ( Karibu uulize!)
Mwanafunzi: Hal shuftum a'qlal ustaadh?! (JE MLISHAONA AKILI YA MWALIMU?!)
Wanafunzi wote . Laaa!
( Hapana!!)
Mwanafunzi : Idhan, Al ustaadhu majnoun!! ( KWAHIYO MWALIMU NI MWENDAWAZIMU?!)
Wanafunzi wote : Ee na'am
( NDIYOOO!!)
Kwa sababu nchi nyingi za kiarabu hawaruhusu mwanafunzi kuchwapwa viboko na mwalimu yoyote, na mwalimu yoyote haruhusiwi kuingia darasani na fimbo , Mwalimu yule alikusanya vifaa vyake vya kufundishia na kwenda ofisini kwa mudiyru ( Mkuu wa shule) kushitaki kwamba wanafunzi wamemtukana.
Nachotaka tujifunze toka kwenye hoja ya mwanafunzi aliyeuliza swali ni kwamba sio kila kisichoonekana kuwa maana yake hakipo.!
Tukimkufuru Allaah kwa hoja kwamba hatumuamini kwa sababu hatujawahi kumuona tutalazimika kukataa uwepo wa vitu vingi ambavyo tunaamini vipo japokuwa hatujawahi kuviona kwa kuwa ni vitu vinaonekan kwa kutumia akili na fikra sahihi!
Vitu hivyo ni kama akili yenyewe, njaaa, furaha, huzuni, mawazo, roho nzuri na roho mbaya na kadhalika. Wawezasikia watu wanasema " Yule jamaa ana roho nzuri au ana roho mbaya" lakini je roho nzuri waweza kuiona, kuigusa, kuinusa, au kuisikia ?!
ITAENDELEA.....