Je, mwanamke anayejifungua kwa upasuaji ana uwezo wa kujifungua watoto wangapi?

gosikulu

Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
71
Reaction score
51
Kama title inavyoeleza, naomba kujulishwa mwanamke anayejifungua kwa upasuaji ana uwezo wa kujifungua watoto wangapi kwa njia hiyohiyo?
 
Nnavyojua mim ni watatu, ila kuna rafki angu mke wake amejifungua watoto5 wanne kwa operation na mmoja wa mwisho amejifungua kawaida, ila alitaftwa na polisi akatembea
 
Ohooo na POLISI tena kwani ni uhalifu
operesheni ni 4 mpaka wa leo nijuavyo
 
kifupi anaweza kujifungua wengi tu kama usalama wa kiafya kwa mama ukizingatiwa.
Ila kwa utaratibu (sio sheria) wa sasa yaani mpya, upasuaji kwa sababu za uzaji mwisho mara mbili (hapo elewa sijasema mwisho watoto wawili, ila upasuaji ndio mwisho mara 2), yaani mama akijifungua kwa upasuaji leo anatakiwa kupewa elimu kuwa kama ikitokea akijigungua kwa upasuaji tena katika mimba inayofuata basi ndio iwe mwisho aombe kufunga kizazi, hii ni kwa ajili ya usalama wake yeye.
 
Hahaha jamaa hajarudi?
Nnavyojua mim ni watatu, ila kuna rafki angu mke wake amejifungua watoto5 wanne kwa operation na mmoja wa mwisho amejifungua kawaida, ila alitaftwa na polisi akatembea
 
kifupi anaweza kujifungua wengi tu kama usalama wa kiafya kwa mama ukizingatiwa.
Ila kwa utaratibu (sio sheria) wa sasa yaani mpya, upasuaji kwa sababu za uzaji mwisho mara mbili (hapo elewa sijasema mwisho watoto wawili, ila upasuaji ndio mwisho mara 2), yaani mama akijifungua kwa upasuaji leo anatakiwa kupewa elimu kuwa kama ikitokea akijigungua kwa upasuaji tena katika mimba inayofuata basi ndio iwe mwisho aombe kufunga kizazi, hii ni kwa ajili ya usalama wake yeye.
Wawili tu?? Kwa usalama wake?? Nini hatari ta kuendelea kuzaa?
 
Binafsi nimeona mama amejifungua kwa operation mara tano na yupo salama mpaka hivi ninavyoandika hapa..

Kusema kweli kibinadamu hatuko sawa..kwa hiyo kinachozingatiwa ni uimara wa kizazi cha mama kuweza kuhimili makovu yatokanayo na operations hizi..

Namanisha nini? Jinsi kizazi kinavyokuwa na makovu mengi ndivyo na uimara wake unavyopungua..kuna mama mwingine hata kufanyiwa mara mbili tu,kizazi unakikuta kimechoka sana..so,kivyovyote vile kumruhusu kuendelea kushika mimba ni kumweka ktk hatari kubwa..

Kwa uzoefu na simple majority, wamama wengi wanaweza kuhimili operations 2 - 3, na pengine labda ndipo hiyo perception ya operations 2 au 3 linapotokea..ila ukirudi kwenye uhalisia,swala hili linategemea namna gani kizazi kinahimili makovu yatokanayo na operations..

Lakini kama tungezingatia hatari kubwa inatokanayo na makovu haya,mjadala wetu usingekuwa mara ngapi mama anatakuiwa kupasuliwa! Pengine labda tungejikuta tunakubaliana kwamba labda mama akishajifungua kwa operation asirudie tena!!

Ni vema tufahamu kwamba,kwamba mshono/kovu likifumuka,mtoto anatoka ndani ya kizazi,anaelea tumboni kwa mama,na damu nyingi inamwagika ndani kwa ndani..ktk mazingira kama haya,hatuzungumzii tena kukosa mtoto(maana hawezi kusurvive hata kwa dakika chache) bali kwamba kama tutachelewa kuchukuwa hatua stahiki,tutamkosa na mama pia..

Mara nyingi kupasuka kwa mshono hutokea mama anapokuwa ameanza uchungu..sasa fikiria mama ananza uchungu akiwa mbali na hospitali!

Na bahati mbaya asilimia kubwa ya wamama hawana uhakika na lini mara ya mwisho kuona siku zao za hedhi na hii huleta tabu ktk makadirio ya siku za kujifungua! Kwa hiyo mama anataja tarehe yoyote tu ilimradi kujibu swali aliloulizwa klinik..matokeo yake ni makadirio ya uongo..na mbaya zaidi mama anazingatia tarehe hii ya kujifungua ambayo ni ya uongo!

Sasa fikiria mama anazingatia tarehe ya uongo,anaendelea na shughuli zake,mimba inafika wakati wa kujifungua,mama hana habari(maana tarehe ya makadirio bado sana)..uchungu unamuanza yupo shambani,safarini,harusini...mshono unaachia!!! Hivi kuna maana hapa kuendelea kubishana idadi ya operations jamani?!!
 
Niliweka mpaka maelezo ya ziada kwenye mabano lakini umeshindwa kuelewa mbona no tatizo. Sijasema wawili, nimesema mara 2, hebu soma tena mkuu.

Madhara pitia comment ya mdau hapo juu pia, ishu kubwa ni kuhofia mfuko wa uzazi kupasuka wakatiwa wa ujauzito hasa mama akiwa kwenye uchungu maana unakuwa umelegea kwa makovu.

Nb: kovu likipata muda mrefu wa kupona linakuwa si hatari sana, ila tahadhari ni bora kuliko baya litokee.
 
Thanks sana mkuu usichoke kuelezea watu wanahitaji elimu mkuu
 
Binafsi nimeona mama amejifungua kwa operation mara tano na yupo salama mpaka hivi ninavyoandika hapa..

Kusema kweli kibinadamu hatuko sawa..kwa hiyo kinachozingatiwa ni uimara wa kizazi cha mama kuweza kuhimili makovu yatokanayo na operations hizi..

Namanisha nini? Jinsi kizazi kinavyokuwa na makovu mengi ndivyo na uimara wake unavyopungua..kuna mama mwingine hata kufanyiwa mara mbili tu,kizazi unakikuta kimechoka sana..so,kivyovyote vile kumruhusu kuendelea kushika mimba ni kumweka ktk hatari kubwa..

Kwa uzoefu na simple majority, wamama wengi wanaweza kuhimili operations 2 - 3, na pengine labda ndipo hiyo perception ya operations 2 au 3 linapotokea..ila ukirudi kwenye uhalisia,swala hili linategemea namna gani kizazi kinahimili makovu yatokanayo na operations..

Lakini kama tungezingatia hatari kubwa inatokanayo na makovu haya,mjadala wetu usingekuwa mara ngapi mama anatakuiwa kupasuliwa! Pengine labda tungejikuta tunakubaliana kwamba labda mama akishajifungua kwa operation asirudie tena!!

Ni vema tufahamu kwamba,kwamba mshono/kovu likifumuka,mtoto anatoka ndani ya kizazi,anaelea tumboni kwa mama,na damu nyingi inamwagika ndani kwa ndani..ktk mazingira kama haya,hatuzungumzii tena kukosa mtoto(maana hawezi kusurvive hata kwa dakika chache) bali kwamba kama tutachelewa kuchukuwa hatua stahiki,tutamkosa na mama pia..

Mara nyingi kupasuka kwa mshono hutokea mama anapokuwa ameanza uchungu..sasa fikiria mama ananza uchungu akiwa mbali na hospitali!

Na bahati mbaya asilimia kubwa ya wamama hawana uhakika na lini mara ya mwisho kuona siku zao za hedhi na hii huleta tabu ktk makadirio ya siku za kujifungua! Kwa hiyo mama anataja tarehe yoyote tu ilimradi kujibu swali aliloulizwa klinik..matokeo yake ni makadirio ya uongo..na mbaya zaidi mama anazingatia tarehe hii ya kujifungua ambayo ni ya uongo!

Sasa fikiria mama anazingatia tarehe ya uongo,anaendelea na shughuli zake,mimba inafika wakati wa kujifungua,mama hana habari(maana tarehe ya makadirio bado sana)..uchungu unamuanza yupo shambani,safarini,harusini...mshono unaachia!!! Hivi kuna maana hapa kuendelea kubishana idadi ya operations jamani?!!
asante sana mkuu kwa maelezo mazuri umewaokoa wengi ila nina swali zaidi KWANINI WAMAMA WENGI WANAJIFUNGUA KWA OPERATION SIKU HIZI KULIKO MWANZO?
 
Sababu ni nyingi.
Mojawapo ni kuongezeka kwa vituo vinavyotoa huduma ya upasuaji..tofauti na zamani,kwa sasa karibu kila wilaya ina hospitali na vituo vya afya kadhaa vyenye uwezo wa kutoa huduma hii.

Pili ni kuongezeka kwa elimu ya afya kwenye jamii.. Watu wameelimika kiasi juu ya madhara ya kuzalia nyumbani. Wamama wanafika mapema hospitali,hivyo ni rahisi kugundua mapema dalili mbaya wakati wa labor na kuchukua hatua stahiki mapema..

Msukumo wa serikali kwa jamii na wahudumu wa afya..kwanza ifahamike kwamba, kama kifo aidha cha mama au mtoto kikitokea wakati wa labor,kinatolewa taarifa wilayani ndani ya siku moja na kutolewa maelezo ni kwa mini kimetokea,je kuna unzembe wowote..sasa, kwa vyovyote vile hata kama ni wewe uko zamu,usingependa hilo likukute,so manesi na waganga wako makini sana kuepuka usumbufu..kwa hiyo wakiona dalili mbaya wakati wa uchungu njia sahihi ni operation, mama anakabidhiwa mwanae kiroho safi,kila mtu anapambana na hali yake!

Urahisi wa upatikanaji taarifa,unafanya jamii kuona kama operations zimezidi! Zamani kama ndugu yako hajajifungua kwa operation ulikuwa vigumu kujua ukubwa wa jambo hili..kitu ambacho watu hawajali ni kwamba hakuna anayezingatia ni wamama na watoto wachanga wangapi walipoteza maisha wakati wa kujifungua! Hawa walikufa aidha kwa kujifungulia nyumbani, au hospitali kwa kukosa huduma ya upasuaji..

Sababu nyingine ambayo tunaweza tusikubaliane nayo hapa ni kwamba,wadada wetu siku hizi(ingawa si wote) si wavumilivu wa uchungu! Kuna mdada akiingia tu labor,utasikia anasema, "nesi/doctor, sins nguvu kabisa,sitaweza kujifungua kawaida". Maana yake huyu ameishajikatia tamaa,vyovyote vile iwavyo,psychologilly ameishaweka inhibition kichwani,kitendo ambacho kinaathiri kabisa mwenendo wa uchungu..huyu hata umpe siku mbili hatajifungua kawaida..hata akijifungua atapata mtoto mfu,au zezeta!

Kiukweli sababu ni nyingi..kuna za kitaalam na kuna za kisiasa..lakini mwisho wa siku,kama mama amezaa kwa operation na akapata mtoto mwenye afya njema naye akabaki salama,ni jambo ya kumshukuru Mungu.

Laiti kama tungejuwa idadi ya watoto mazezeta tulionao majumbani mwetu na usumbufu wanaopata wazazi wao kuwalea..na laiti kama tungejua kama sababu kubwa ya kutokea kwa watoto hawa ni mama kulazimishwa kujifungua kawaida ktk mazingira ambayo operation ndiyo ilikuwa njia salama kwa watoto hawa..pengine leo tungekuwa na mtazamo tofauti juu ya kuzidi kwa operations hizi!
 
Nnavyojua mim ni watatu, ila kuna rafki angu mke wake amejifungua watoto5 wanne kwa operation na mmoja wa mwisho amejifungua kawaida, ila alitaftwa na polisi akatembea
Kwa nini polisi wamtafute?
 
Back
Top Bottom