asante sana mkuu kwa maelezo mazuri umewaokoa wengi ila nina swali zaidi KWANINI WAMAMA WENGI WANAJIFUNGUA KWA OPERATION SIKU HIZI KULIKO MWANZO?
Sababu ni nyingi.
Mojawapo ni kuongezeka kwa vituo vinavyotoa huduma ya upasuaji..tofauti na zamani,kwa sasa karibu kila wilaya ina hospitali na vituo vya afya kadhaa vyenye uwezo wa kutoa huduma hii.
Pili ni kuongezeka kwa elimu ya afya kwenye jamii.. Watu wameelimika kiasi juu ya madhara ya kuzalia nyumbani. Wamama wanafika mapema hospitali,hivyo ni rahisi kugundua mapema dalili mbaya wakati wa labor na kuchukua hatua stahiki mapema..
Msukumo wa serikali kwa jamii na wahudumu wa afya..kwanza ifahamike kwamba, kama kifo aidha cha mama au mtoto kikitokea wakati wa labor,kinatolewa taarifa wilayani ndani ya siku moja na kutolewa maelezo ni kwa mini kimetokea,je kuna unzembe wowote..sasa, kwa vyovyote vile hata kama ni wewe uko zamu,usingependa hilo likukute,so manesi na waganga wako makini sana kuepuka usumbufu..kwa hiyo wakiona dalili mbaya wakati wa uchungu njia sahihi ni operation, mama anakabidhiwa mwanae kiroho safi,kila mtu anapambana na hali yake!
Urahisi wa upatikanaji taarifa,unafanya jamii kuona kama operations zimezidi! Zamani kama ndugu yako hajajifungua kwa operation ulikuwa vigumu kujua ukubwa wa jambo hili..kitu ambacho watu hawajali ni kwamba hakuna anayezingatia ni wamama na watoto wachanga wangapi walipoteza maisha wakati wa kujifungua! Hawa walikufa aidha kwa kujifungulia nyumbani, au hospitali kwa kukosa huduma ya upasuaji..
Sababu nyingine ambayo tunaweza tusikubaliane nayo hapa ni kwamba,wadada wetu siku hizi(ingawa si wote) si wavumilivu wa uchungu! Kuna mdada akiingia tu labor,utasikia anasema, "nesi/doctor, sins nguvu kabisa,sitaweza kujifungua kawaida". Maana yake huyu ameishajikatia tamaa,vyovyote vile iwavyo,psychologilly ameishaweka inhibition kichwani,kitendo ambacho kinaathiri kabisa mwenendo wa uchungu..huyu hata umpe siku mbili hatajifungua kawaida..hata akijifungua atapata mtoto mfu,au zezeta!
Kiukweli sababu ni nyingi..kuna za kitaalam na kuna za kisiasa..lakini mwisho wa siku,kama mama amezaa kwa operation na akapata mtoto mwenye afya njema naye akabaki salama,ni jambo ya kumshukuru Mungu.
Laiti kama tungejuwa idadi ya watoto mazezeta tulionao majumbani mwetu na usumbufu wanaopata wazazi wao kuwalea..na laiti kama tungejua kama sababu kubwa ya kutokea kwa watoto hawa ni mama kulazimishwa kujifungua kawaida ktk mazingira ambayo operation ndiyo ilikuwa njia salama kwa watoto hawa..pengine leo tungekuwa na mtazamo tofauti juu ya kuzidi kwa operations hizi!