Je mwongozo wa ada kwa shule binafsi upo wapi?

Je mwongozo wa ada kwa shule binafsi upo wapi?

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,112
Reaction score
4,540
Nakumbuka mara kadhaa Serikali, kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, chini ya Naibu Waziri Bw. Mulugo, iliwahi kutoa tamko ya kwamba itatoa mwongozo wa viwango vya ada kwa shule binafsi, shule itakayotoza zaidi ya viwango hivyo itabidi iombe kibali maalumu kutoka Wizarani.
Kwa sasa zimebaki siku kadhaa kabla ya mwaka kwisha, huu ni wakati bodi za Elimu za shule kadhaa hukaa na kuweka mipango ya fedha (mapato na matumizi). Je bodi hizo zitapanga bila kuwa na uhakika wa mapato?. Nasema hivyo kwa kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa shule nyingi ni michango ya ada.
Pia huu ndio wakati ambao wazazi huweka bajeti na kujiandaa na utekelezaji wa mipango ya elimu wa watoto wao, je awzazi/walezi watapanga bila ya kuwa na viashiria vya gharama Serikali ilivyoahidi itatoa?
 
Back
Top Bottom