Je, na hawa dagaa wa kwenye pakiti wachungu kama klorokwini wanahifadhiwa na nini?

Je, na hawa dagaa wa kwenye pakiti wachungu kama klorokwini wanahifadhiwa na nini?

blogger

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
12,112
Reaction score
15,060
Ndugu zangu ifike mahala tuweke siasa pembeni sayansi ifanye kazi. Nampongeza sana Makamu wa Rais kulipua hili jipu. Tunalishwa sana sumu.

Kuna hawa dagaa wa pakiti ambao wanaonekana wemekaangwa huko walikotoka. Dagaa hawa ni wachungu sana kama klorokwini, hata uoshe vipi! Alafu ukila wanasababisha koo kuwasha na mafua.

Hawa wanahifadhiwa na nini!? Mamlaka husika embu fanyeni kazi yenu.

Kuna hawa samaki wa mtera, samaki hawa wanapigwa dawa hadi wanabadilika rangi wanakuwa weusi. Unaweza ukafikiri ni sato kumbe ni pegere. Ukila unabaki na mafua na koo kuwasha. Tuache siasa tunaumizana. Uchunguzi wa kisayansi ufanyike kwa mazao ya majini.
images.jpeg
 
Unasema tuweke siasa pembeni sayansi ifanye kazi halafu hapo hapo unampongeza makamu raisi kwa kulipua bomu wakati hana evidence ya kuback up alichosema na aliyasema pasipo kuwa na ushahidi wa kisayansi.
Sasa hapo tuelewe lipi
 
Ametoa way forward.. uchunguzi wa kitaalamu ufanyike.. lakini uchunguzi wa nini ....mi hapa nna mafua makali nimekula hivyo vidagaa jana
 
Ametoa way forward.. uchunguzi wa kitaalamu ufanyike.. lakini uchunguzi wa nini ....mi hapa nna mafua makali nimekula hivyo vidagaa jana
Sie tunanunua wabichi tunakaanga sio wachungu na hatupati mafua labda hao mnaoletewa huko
 
Dagaa wa Ziwa Nyanza (Victoria) huwa wachungu miaka yote ila ni vema tu sampuli zao zipelekwe maabara yetu na zingine zipelekwe maabara za nje ya Nji

Hata matunda aina apples yanayoingizwa Nchini hupakawa dawa ili yang'ae yenyewe pia yafanyiwe uchunguzi.

Ushauri wangu follow your instinct.
 
Ametoa way forward.. uchunguzi wa kitaalamu ufanyike.. lakini uchunguzi wa nini ....mi hapa nna mafua makali nimekula hivyo vidagaa jana
Kwa hiyo wewe ukiwa na mafua baada ya kula dagaa maana yake hao dagaa wamehifadhiwa kwa maji ya maiti?

Mbona hoja zako zinapingana na sayansi maana unafikia conclusion pasipo huo uchunguzi kufanyika.

What if wanahifadhiwa kwa dawa tofauti na maji ya maiti?
 
Ziwa Nyanza/Victoria kwa sasa limezungukwa na Migodi mikubwa na midogo midogo mingi, Kemikali zinaingia Ziwani kipindi cha masika ni nyingi, na sasa Cynanide nayo inatumiwa na Wavuvi haramu.

Samaki wa Tanganyika sawa na hata Nyasa sawa lakini Victoria/Nyanza ni kula kwa hamu tu.
 
Ziwa Nyanza/Victoria kwa sasa limezungukwa na Migodi mikubwa na midogo midogo mingi Kemikali zinaingia Ziwani kipindi cha masika ni nyingi na sasa Cynanide nayo inatumiwa na Wavuvi haramu.

Samaki wa Tanganyika sawa na hata Nyasa sawa lakini Victoria/Nyanza ni kula kwa hamu tu.
Sawasawa..🙏🙏💯
 
Hata Bahari zetu ziko Polluted hata mabwawa ya kufugia Samaki wanatumia kemikali.

Asilimia kubwa ya Samaki kwa sasa sio chakula salama ni bora Senene na Kumbikumbi ambao ni good source of protein.
 
Kwani uchungu wa dagaa si waletwa na kutotolewa kwa sehemu ya utumbo wake?
 
Mpikaji mwambie atie maziwa fresh badala ya maji ya mchuzi hutasikia uchungu
 
Bado ninawaza hivi lengo haswa la makamu wa rais ilikuwa ni kuleta taharuki au nini haswa!!
 
Dagaa wa Ziwa Nyanza (Victoria) huwa wachungu miaka yote ila ni vema tu sampuli zao zipelekwe maabara yetu na zingine zipelekwe maabara za nje ya Nji

Hata matunda aina apples yanayoingizwa Nchini hupakawa dawa ili yang'ae yenyewe pia yafanyiwe uchunguzi.

Ushauri wangu follow your instinct.
Bora yapelekwe maabara ya nje na sio hapa nchini

Hapa nchini hapaaminiki kabisa aisee, RUSHWA nje nje.
 
Back
Top Bottom