Je na hili ni la kusingiziwa kwa waandaaji wa Miss Tanzania au?

Je na hili ni la kusingiziwa kwa waandaaji wa Miss Tanzania au?

HOBBIES

Senior Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
145
Reaction score
17
Dar es Salaam. Kashfa imemwandama Miss Tanzania 2014, Sitti Mtevu baada ya vielelezo mbalimbali kuonyesha kuwa ameghushi umri.

Sitti katika fomu zake alijaza ana miaka 18, kitendo ambacho kimewashtua watu wengi na kuanza kufuatilia taarifa zake na kubaini kuwa kumbe ana miaka 25.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, mrembo huyo aliyetokea Kanda ya Temeke hakuwa na sifa za kushiriki mashindano kwa vile tayari alishavuka umri uliowekwa kikanuni na waandaaji wa shindano hilo.

Sifa za mshiriki wa Miss Tanzania, anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 23, awe raia wa Tanzania, awe hajaolewa, awe na ufahamu wa kutosha wa kujieleza, awe hajazaa, asiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.

Pia, asiwe ameshiriki mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi yoyote zaidi ya mara moja kwa mwaka husika, maana yake hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja. Lugha inayotumika ni Kiswahili na Kingereza.

Lakini, katika hali ya kushangaza, licha ya mrembo huyo kukiuka masharti hayo, alitangazwa kuwa Miss Tanzania mwaka huu, ushindi ambao umezua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiponda ushindi wake na wengine wakienda mbali na kudai mrembo huyo ana mtoto.

Mastaa mbali mbali wame
toa matamko yao kwenye mitandao ya kijamii wakiponda ushindi huo na kuilaumu Kamati ya Miss Tanzania kuvurunda.

Mwanamitindo Martin Kadinda alisema: “Uncle Lundenga nakuheshimu na ninakuamini, lakini katika hili sikuungi mkono.”

Mtayarishaji wa kipindi cha Diaspora, Jestina George alisema:
“Jamani eee uongo kila mtu anadanganya na makosa wote tunafanya mimi bado nawalaumu viongozi wa Miss Tanzania maana naamini asilimia 100 walilijua hili toka mwanzo. Sitti mama pole.”

Akizungumzia suala hilo, mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema: “Ni changamoto kubwa, lakini naamini ndio kukua kwa mashindano, mwaka jana na juzi walisema shindano limedoda, mwaka huu wanalizungumzia wiki nzima, acha watu waseme ni upepo tu utapita.”

Meneja wa Redd’s, wadhamini wa mashindano hayoilo, Victoria Kimaro alisema: “Kwa kweli maneno yamekuwa mengi, ya kweli na uongo, lakini naamini mengi ni ya uongo, siku yoyote kuanzia sasa Sitti atazungumza.
 
baada ya kupata habari hii nimekuwa nikijiuliza sana hivi kwa nini sisi watanzania tumekuwa tunasingizia kuonewa na kusemewa uongo hata kwenye mambo ambayo ni dhahiri kwamba tumefanya makosa!!!!
 
Lundenga hana hoja, shindano kuzungumziwa wiki nzima kwake ndio mafanikio? Eti ni upepo? Anatakiwa kujibu hoja.

Na huyo meneja wa redd's atuambie ya kweli ni yapi na uongo ni yapi. No longolongo.
 
Nimeona miss Kennya nae et ana miaka 19 ana degrer,masters na phD sio bongo tu kumbeee hhhhaaaaa
 
kuna mida napata shida kujua neno "star" linamaanisha nini, Jestina george, star; martin kadinda star. what have they done to be referred as such? are they really so, or just individuals who happen to be "popular". The more wema have sex scandals the more martin's name is heard on public (how he manage her sex life I guess ), and Jestina, she appears on Lemutuz blog couple of times, le mbebs mkalez!
 
Lundenga hana hoja, shindano kuzungumziwa wiki nzima kwake ndio mafanikio? Eti ni upepo? Anatakiwa kujibu hoja.

Na huyo meneja wa redd's atuambie ya kweli ni yapi na uongo ni yapi. No longolongo.

andaa kalamu yako camera na karatasi jummane njoo lamada pale kuna press conference mjiandae kupokea sound takatifu zilizopangwa zikapangika lazima muwe wapole tu
 
andaa kalamu yako camera na karatasi jummane njoo lamada pale kuna press conference mjiandae kupokea sound takatifu zilizopangwa zikapangika lazima muwe wapole tu

ndo maana yake kama ulimsikiliza lundenga akihojiwa na sam misago ktk fridaynight live alisema jumanne watazungumza na ndo itakuwa mwisho wa hii inshu sound tebe hapo
 
kuna mida napata shida kujua neno "star" linamaanisha nini, Jestina george, star; martin kadinda star. what have they done to be referred as such? are they really so, or just individuals who happen to be "popular". The more wema have sex scandals the more martin's name is heard on public (how he manage her sex life I guess ), and Jestina, she appears on Lemutuz blog couple of times, le mbebs mkalez!

Hoja nzito sana hii,ni ukweli mtupu!!ebu iwekee uzi wake.
 
kuna mida napata shida kujua neno "star" linamaanisha nini, Jestina george, star; martin kadinda star. what have they done to be referred as such? are they really so, or just individuals who happen to be "popular". The more wema have sex scandals the more martin's name is heard on public (how he manage her sex life I guess ), and Jestina, she appears on Lemutuz blog couple of times, le mbebs mkalez!

Kuwa star uchwara Tanzania siyo ishu. Wewe kunya hadharani au umtafute mtu wa kugombana naye FaceBook au Insta, believe me utajulikana tu. Jiulize kale kajamaa Martin au Jestina wana ustaa gani. Star bongo?
 
Daa naipenda sana nchi yangu.narudia tena naipenda sana Tanganyika
 
kuna mida napata shida kujua neno "star" linamaanisha nini, Jestina george, star; martin kadinda star. what have they done to be referred as such? are they really so, or just individuals who happen to be "popular". The more wema have sex scandals the more martin's name is heard on public (how he manage her sex life I guess ), and Jestina, she appears on Lemutuz blog couple of times, le mbebs mkalez!

Let me tell u one thing,in tz if u associate urself with right people(in limelight) at the right tyme overnight u will become super star mifano ipo kedekede Vanessa ni superstar,Masogange ni Superstar,Jaja ni super star,sitti mtemvu,bibi bomba,Diva loveness, its just a matter of timing na watu unaojiassociate nao even u may become bongolala superstar
 
kuna mida napata shida kujua neno "star" linamaanisha nini, Jestina george, star; martin kadinda star. what have they done to be referred as such? are they really so, or just individuals who happen to be "popular". The more wema have sex scandals the more martin's name is heard on public (how he manage her sex life I guess ), and Jestina, she appears on Lemutuz blog couple of times, le mbebs mkalez!

The way a star or a celebrity is defined in Bongo is unique and is quite different from the rest of the world. Elsewhere, a star is a person of means - not necessarily rich but not a pauper for sure. Only in Bongo a scandalous and a poor person is considered as a star. Most of them survive as "Matonya" or beggars to be honest. Any musician, actor or actress is a star or celebrity in Bongo. To the list add whoever has participated in a beauty content at any level! A scandal of any kind adds credibility to their celebrity status. We have a long way to go!
 
Back
Top Bottom