Kwa mujibu wa nadharia hii ni kwamba kwa kila tendo liwe zuri au baya utapokea malipo yake hapahapa duniani kabla haujafa. Kwa baadhi ya watu nadharia hii inafanya kazi ila kwa watu wengine inakataa kwa nini?
Kwa mfano viongozi wa nchi ya Marekani wameamrisha mauaji ya watu wengi duniani, wamesababisha vita visivyoisha sehemu nyingi. Nchi nyingi zimesambaratika watu wake wanaishi maisha dhiki kuu. Labda ungetegemea karma iwashugulikie na wao wapate misukosuko au hata kurukwa na akili kwa wingi wa damu walizo mwaga lakini wapi, yaani wanaishi maisha mazuri yenye starehe nyingi tena wanaishi umri mrefu hadi miaka 90.
Mfano mwingine, kwenye ukoo wenu wale ndugu wenye roho nzuri za kusaidia wenzao kwa huruma na upendo huwa na maisha magumu tena ya kawaida tu. Lakini wale wachache wenye uwezo wanaweza kuwa wabinafsi wanojijali wao yani mtu anaweza ugua asitoe msaada mpaka mgonjwa akafa ndo anatoa msaada wa mazishi.
Cha ajabu mtu huyu anaendea na maisha yake vizuri na watoto wake watafika hadi chuo kikuu na badae kupata nzuri. Nyie wenye roho za kusaidiana mnaendelea na maisha yenu ya kuunga unga.
Mfano wa mwisho, Tanzania ilisaidia nchi nyingi kupata uhuru kama vile Afrika kusini, Angola, Zimbabwe, Namibia na Msumbiji. Ungetegemea Karma iibebe Tanzania kwa wema wake lakini tumeendelea kuishi maisha magumu ya kimasikini tena tukipitwa kiuchumi na nchi tulizo zisaidia!
Je, hii nadharia ina ubaguzi katika malipo? Naomba majibu yenu wadau.
cc Pascal Mayalla, Mshana Jr r, GENTAMYCINE na wajuzi wengine wa JF.