ni kweli mkubwa nafsi kupitia maumbile zina madaraja mbalimbali,wako watu wanapata ndoto za kweli kama taarifa ya tukio linalotarajiwa,wengine bila hata kuota bali wazo lolote litalomjia bila shinikizo huwa ni taarifa ya kweli,wako pia ambao akikuapiza au kukulaani kwa chochote hutokea kweli,hivi ni sehemu ndogo ya vipawa ambavyo baadhi ya binadamu wamepewa.ndipo wengine wakishajigundua kuwa na mambo kama haya hujifanya waganga kuibia watu.haya ni mambo ambayo manabii walipewa rasmi kabisa kuwa nayo na ndio chimbuko la miujiza,lakini hata watu wa kawaida hubahatika kuwa na baadhi ya mambo.