Je, nahitaji kibali kumiliki silaha hii?

FURY BORN

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2020
Posts
638
Reaction score
1,150
Hii kitu nayo nahitaji kibali kwa maana ya licence to carry or licence to own. Wazee wa kamati ya ulinzi na usalama tukumbudhane, nataka kuagiza kwa mchina, manake majuzi vibaka wameua mbwa wangu na wakaingia uani na kukata dirisha, bahati madifisha yangu sikutumia flat bar bali nondo, hivo wakati wanakata nondo ya kwanza nikastuka kuchungulia nikaona wajinga wawili wako nje wamevaa vichupi tu.

Bahati mbaya ndani nina panga tu. Nikapuliza filimbi wakakimbia. Lkn ningekuwa na hii kitu ningewamwaga wote kimya kimya.

 
Tunakoelekea silaha za jadi zitasajiliwa na kuwa na vibali.

Fuatilia hill mkuu, ukizingatia huo Upinde ni Modern
 
U
Tatizo wabongo mkipewa mnaenda kutambia baa, tumieni tu 'topito' ndo mliyozoea wakati mnakua mlitumia kuwindia ndege....
Ukikuwa utaelewa kwa sasa malizia kucheza game hapo sebuleni kwa shemeji yako. Ila kumbuka ulipaswa kumwonea dadako huruma anapofunga mlango usiku yanayompata huko yeye ndo anajua.
 
U

Ukikuwa utaelewa kwa sasa malizia kucheza game hapo sebuleni kwa shemeji yako. Ila kumbuka ulipaswa kumwonea dadako huruma anapofunga mlango usiku yanayompata huko yeye ndo anajua.
Nikikua nitaelewa kutamba baa na silaha ya moto? wee jamaa unaonekana kilaza sana.....tafuta topito, hizo silaha watamiliki wenye akili timamu....
 
Wategee upupu
 
Wategee upupu
Nilifikiria kununua alarm system ya pilipili lkn ile ina tatizo moja ukisha arm system ikitokea false alarm inamwaga pilipili nyumba nzima. Lakini pia wakivunja ikimwaga pilipili sebuleni wewe pia huwezi toka chumbani japo watakuwa hawaoni hivo nawe hutoweza kutoka kuwapa kisago
 
Nikikua nitaelewa kutamba baa na silaha ya moto? wee jamaa unaonekana kilaza sana.....tafuta topito, hizo silaha watamiliki wenye akili timamu....
Ndo maana nikakwambia ukikuwa utaelewa kwa sasa huwezi elewa, kajifunze kwanza kiswahili hamna neno topito kwa kiswahili. Isipokuwa huko kwenu majita. Na wajita wengi ujuaji ndo unawasumbua na ndo maana ukienda mkoa mzima wa mara na Tanzania kwa ujumla hakuna mjita milionare. Kwa sababu ya kujimwambafai.
 
IGP alishasema wanaume tuache umama, mwanaume unakosaje rungu,sime,manati,nondo nzito ama silaha yoyote ya kujihami pindi unapokutana zahama ndogondogo kama za kuingiliwa na vibaka?

Kumbuka silaha zote zisizo za moto hazihitaji kibali chochote, ikiwemo upinde na mishale.
 
Sawa dada, kumbe hujui kiswahili kinaundwa pia na mchanganyiko wa maneno ya kibantu na bado maneno yake na misamiati inazidi kuzaliwa kila kukicha......sasa kama hujui maana ya neno topito wewe utakuwa ni kiazi hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…