Kuna zile series zinazowekwaga kwa server moja kwa moja, tunazozipata kwa kuandika index of (jina la movie) zilikuwa zinagoma kupakuliwa kwa njia tuliyozoea zamani, kuwa ukii-click tu basi inaanza kuteremka.
Nimepata ujuzi kwenye mtandao nikadownload Application inaitwa JDownloader 2 hapa
JDownloader.org - Official Homepage , aisee inapakua kila kitu. Binafsi huwa napenda hizi za index maana bapata zenye resolution ndogo (480p) zikiwa pia na ukubwa mdogo ambapo kwangu zinanifaa kabisa kutazama tofauti na torrent ambako files nyingi huwa zina ukubwa mkubwa na resolution kubwa pia. Unachofanya baada ya kuinstall hiyo application, ni kufuungua application iwe inarun halafu unakopi link yenye directory uitakayo kwenye browser, application itadaka link hiyo automatically au wewe mwenyewe utaenda kwenye tab ya linkgrabber na utabonyeza alama ya kujumlisha link itajipest halafu italeta unavyotaka kudownload, utaweza kuvipunguza usivyotaka kwa kufuta manually na baada ya hapo unabonyeza alama ya PLAY, mzigo unaanza kushuka.
View attachment 1393324