Je,naweza kuibiwa pesa benki kwa mtu kujua namba yangu ya siri?

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
2,133
Reaction score
661
Jamani naombeni msaada wa haraka,nilienda kutoa pesa kwenye ATM ya CRDB na palikuwa na mtu ambaye alinielekeza mambo flani,na huyu mtu aliona namba yangu ya siri,je ataweza kuniibia kwa namna yoyote pesa zilizobaki? Naomba mnifahamishe kwa hili,ili kama kuna madhara yanayoweza kutokea niwasiliane na CRDB wanisaidie kuiblock hadi wanitengenezee namba mpya.
NATANGULIZA SHUKRANI.
 
we kwa nini ulimuonyesha namba yako ya siri..? ndio anaweza kukuibia....tena inawezekana mpaka saa hii keshaiba.....
kwenda badilisha password pale pale kwenye atm machine.....kabla hajawaambia na marafiki zake......
 
ooh mungu wangu,kuna option ya kubadili namba ya siri hapohapo?
 
Kadi yako uko nayo hapo? Kama kadi unayo hawezi kukuibia ila kama na kadi ulimuachia huna hata haja kuuliza hapa kitakachotokea.

Sio lazima akuibie lakini, bado kuna watu wazuri tu duniani na pengine alikusaidia kwa uzuri tu.
 
Kwani huyo mtu amekaa kiwizi wizi mpaka unamhisi hivyo?
 
Mtu akiona pin number yako hawezi kukuibia tu hivi hivi labda awe na kadi yako ya bank. Bt ni vizuri wanasemaga kubadilisha pin number yako from time to time hata kama hakuna aliyeiona
 
kama hana kadi yako sio rahisi kuibiwa
labda ingekuw amekusaidia onilne transaction lakini kama ni ATM huna haja kuogopa
sio kila mtu mwizi hata mm nshasaidia wengi tena wazee ktk ATM
jijenge utaratibu wa kubdaidli namba yako ya siri kila mara.
 
akijua pin yako anaweza kukuibia kwa kutumia sim banking as long as anajua na namba yako. Mimi nilishawahi pata matatizo makubawa kwa mambo haya. Badili password fasta.
 
Ushauri mzuri sana, kila mara kuna haja ya kubadili pin yako.
 
Asanteni wote kwa ushauri,niliwahi haraka nikabadili namba ya siri. Sio kwamba jamaa alikuwa amekaa kiwizi,lakini nilikosa amani moyoni na ukizingatia hapa ni mjini( Arusha),nikaona niombe ushauri kabla chochote hakijanitokea.
 
Kadi yako uko nayo hapo? Kama kadi unayo hawezi kukuibia ila kama na kadi ulimuachia huna hata haja kuuliza hapa kitakachotokea.

Sio lazima akuibie lakini, bado kuna watu wazuri tu duniani na pengine alikusaidia kwa uzuri tu.

Yap! Kadi nilikuwa nayo,nashukuru kwa ushauri. Nimeshaibadilisha lakini.
 
Mtu akiona pin number yako hawezi kukuibia tu hivi hivi labda awe na kadi yako ya bank. Bt ni vizuri wanasemaga kubadilisha pin number yako from time to time hata kama hakuna aliyeiona

nashukuru sana kwa ushauri.
 
Nyie mnaosema hawezi kuibiwa bila huyo mtu kuwa na kadi yake, kwani hamjasijiaga za watu kutumia kamera kupiga picha kadi au kurekodi ka video esp kwa sasa inafanywa sana na vi mobile phones. Mtu anashika unadhani ni kashika tu simu yake mkononi kumbe anaiba mambo. Then baadae wanatengeneza kadi na info hizo then inalala kwako.

Online shopping nayo itamsaidia kutumia pesa bila kadi, etc. Unless kama kuna security kali inayoomba details zingine za mwenye nayo.

Ndio maana ni muhimu sana kufunika kwa mikono kwa kuficha wakati unaweka pin namba yako.
 
akijua pin yako anaweza kukuibia kwa kutumia sim banking as long as anajua na namba yako. Mimi nilishawahi pata matatizo makubawa kwa mambo haya. Badili password fasta.

pole sana kwa matatizo yaliyokupata. Nimeshabadili password.
 
Nasikia kuna card skimmers,what they play wt cards ni kwamba,they plug a magnetic cheap kwenye ATM machines of which unapotumia data zako znabakia pale thn wanacheza na akaunti yako wapendavyo,mytake ni kutojiamini sana kuwa m2 akijua pincode yako hata km hana card anaweza kufanya k2.watu wako very smart na technology!
 
Nyie mnaosema hawezi kuibiwa bila huyo mtu kuwa na kadi yake, kwani hamjasijiaga za watu kutumia kamera kupiga picha kadi au kurekodi ka video esp kwa sasa inafanywa sana na vi mobile phones. Mtu anashika unadhani ni kashika tu simu yake mkononi kumbe anaiba mambo. Then baadae wanatengeneza kadi na info hizo then inalala kwako.

Online shopping nayo itamsaidia kutumia pesa bila kadi, etc. Unless kama kuna security kali inayoomba details zingine za mwenye nayo.

Ndio maana ni muhimu sana kufunika kwa mikono kwa kuficha wakati unaweka pin namba yako.

shukrani kwa elimu yako uliyonipatia,mimi mwenyewe japo sikuwa na uelewa wa kutosha,ila nilikosa amani moyoni ndo maana nikaamua kubadili.
 
Kadi yako uko nayo hapo? Kama kadi unayo hawezi kukuibia ila kama na kadi ulimuachia huna hata haja kuuliza hapa kitakachotokea.

Sio lazima akuibie lakini, bado kuna watu wazuri tu duniani na pengine alikusaidia kwa uzuri tu.

Anaweza kukuibia bila card kupitia SIMBanking. Pia unaweza kubadilisha password bila kwenda ATM kama umejiunga na SIMBanking
 
akijua pin yako anaweza kukuibia kwa kutumia sim banking as long as anajua na namba yako. Mimi nilishawahi pata matatizo makubawa kwa mambo haya. Badili password fasta.

Kama ni kweli mtu anaweza ibiwa hela kisa ana pin number yako basi bongo tuko nyuma sana.. Mtu inabidi ajue full name
yako address na bank account or Card number kuweza kufanya chochote.. Msije mkawa mnaibiwa na wafanyakazi wa bank nyie mkadhani ni watu wa nje
 
Back
Top Bottom