kabiriga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 1,109
- 1,171
Kuna kampuni nyingi za simu hapa Tanzania lakini kuna mambo yanawafanyia wateja wao sio fare kabisa,mfano baadhi ya makampuni yana huduma ya internet kwa malipo ya kabla ya kununua kifurushi kwa kwa muda fulani mfano,siku,week,mwezi nk lakini unakuta umeishanunua kifurushi na matatizo ya mtandao wao yanatokea ndani ya siku kama tatu hivi,hakuna hiyo huduma na wakati umeishalipia na kibaya zaidi awafidii hizo siku kwani muda ukiisha na huduma inakwisha.Je naweza kuwashitaki kwa sheria hipi kwani nisawa na wizi kutoa huduma pungufu kwa malipo ya mteja.