Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wanasheria naomba kuuliza. Katika kila lita ya petroli au diesel tunayonunua, kuna hela inayokatwa na kwenda TANROADS kwa ajili ya matengenezo ya barabara. Sasa je, ikiwa hiyo hela haitumiki kutengeneza barabara, hadi kuwapo mashimo makubwa barabarani yanayosababisha ajali, naweza kumshtaki Magufuli na TANROADS na kuwadai fidia kwa kuwa mimi nimelipia matengenezo ya barabara lakini wao hawajafanya matengenezo hayo hadi nikapata ajali?