Core ni kma procoessor iliyopo ndani ya CPU. Hizi core ndio zinafanya hzo instructions zinazohitajika kurun program flan. Nguvu ya core inakuwa determined kwa kupima Instructions per cycle (IPC), hii ni idadi ya maelekezo core yako inaweza fanya kwa mzunguko mmoja wa CPU (mzunguko mmoja wa CPU clock speed). IPC ndio muhim sana, core mbili tofaut kutoka processor mbili tofaut zinaweza kuwa na clock speed sawa (mf 1GHz) ila moja ikawa na 2000IPC na nyingine ikawa na 1000IPC ile ya 2000 IPC ndio yenye nguvu. Lakini kumbuka kuwa clock speed bado ni muhimu, kma CPU zote ni za class moja na generation sawa ile yenye clock speed kubwa ndio itakuwa na nguvu zaidi.
Sasa je ni kitu gani kinachangia core/processor kuwa na IPC kubwa kuliko nyingine?
Cha kwanza ni number ya transistors, kila processor ina transistors ndani yake ambazo ndio zinarun hzo instructions. Core moja inaweza kuwa na transistors nyingi kuliko nyingine. Yenye transistor nyingi itakua na IPC kubwa.
Pili ni size ya core hyo. Core kubwa inamaanisha kuwa inaweza beba transistors na nodes nyingi zaidi. Ndio maana zile Xeon processors za kwenye servers zinakuwa na core zenye nguvu sana
Kingine pia ni kwamba fabrication method (njia inayotumika kutengeneza processor) inachangia uwepo wa transistors na nodes nyingi. Kma ukicheki kwenye processor specification utakuta hchi kitu kimenadikwa: 10nm or 7nm or 5nm. Hichi ni kipimo cha udogo wa components (transistors and nodes) zilizopoa kwenye processor. Uwepo wa components ndogo inawezesha kuweka transistors and nodes nyingi kwenye processor yako na kupandisha IPC kwa kila core.
Pia processor zenye clock speed ndogo zinaweza kuwa na IPC kubwa sababu ya joto linalotengezwa. Processor zenye clock speed kubwa zinatengeza joto jingi na hii inalimit ufanyaji kazi wa transistors hvyo kuwa na IPC ndogo. Ila ukiwa na clock speed ndogo unaweza pandisha IPC yako sababu joto sio jingi sana. Ndio maana unakuta 10th gen i3 yenye clock speed ya 1.4ghz inaikalisha 3rd gen i7 yenye clock speed ya 2.7ghz kwenye single core performance.
Ukitaka details zaidi soma hizi sehemu mbil:
1.
2.
Instructions per cycle - Wikipedia
Sent using
Jamii Forums mobile app