Habari Wana jamii,
Upande wa Sheria! Nilimaliza masomo yangu ngazi ya stashahada kwenye chuo kimoja wapo cha serikali hapa jijini dsm mwaka 2016. Tatizo likaja sikuwa nimemaliza ada tena hela nyingi tu na hata nilipotoka field nakuandaa ile field report tukazikusanya kwa msimamizi wetu wa pale chuoni, lakini ukipeleka anakwambia njoo na risiti ya malipo ya ada na kama huna hiyo report siipokei. Mi nikampa mezani pale nikasema ada sijalipa ila nitalipa tu sababu sijapata cheti.
Akaichukua akaiweka, sasa 2017 nimelipa ada yote nilipata mfadhili. Ikanibidi nifuate cheti, nakuta hakuna cheti wala transcript, nikauliza kwa afisa wa mitihani kulikon? Akasema ngoja tutizame faili kisha tutakujulisha sasa tokea pale sikutafutwa mpaka 2020 nilipoenda tena nikakuta hakuna cheti, nikauliza tena sasa ikawa Kama ndo wameniona na kusikia jambo lile kwa mara ya kwanza, nikaacha namba yangu ya usajili na ya simu, napo hawakunitafuta.
Wiki mbili mfululizo zilizopita 2022 nimeenda tena kuchukua nakuta hamna, jibu pia la msingi hakuna yani hamna mtu alofanyia kazi swala lile, nikaenda kwa afisa mitihani nikamkuta mpya nikamueleza shida yangu akasema mwambie mtu wa masijala akuangalizie faili kisha lilete kwangu, hapo ndo tatizo lilipo masijala.
Naambiwa njoo kesho, njoo kesho, njoo kesho mpaka wiki 2 zimeisha na nimechoka. Je naweza kwenda kuwashitaki mahakamani kwa kutonitengenezea cheti changu?