Je, naweza nikapata jicho la bandia? Naweza nikalipata wapi na kwa gharama ya sh ngapi?

Joined
Apr 12, 2013
Posts
63
Reaction score
15
Samahani mimi naishi Mwanza nilipata ajali mwez wa 5 iliyopelekea jicho langu la kulia kutoka nilipelekwa Bugando nikafanyiwa upasuaji likatolewa moja kwa moja, lakini mpaka saivi linatoa machoz kila wakati inayonipelekea kukaa ndani muda wote,

Sasa kuna jamaa ameniambia kuwa kuna macho ya bandia likiwekwa hapatatoa machozi tena,nilipoenda Bugando wamesema iyo huduma hawana.

Sasa kama kuna yeyote anayejua wapi naweza nikamaliza tatizo kama ili samahani naomba anielekeze, kama anajua na gharama aniambie ni sh ngapi?Asanteni


Sent from my Magnus bravoZ10 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana,ila kikubwa uzima.....ngoja waje wanaojua ila unaweza kutumia miwani nyeusi kama haujisikii comfortable kutoka nje unavaa hiyo miwani,pole sana

Sent from my T1-701u using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu,nenda CCBRT Dar,ila madaktari wa siku hizi wana roho mbaya sana,hivi kweli unamfanyia mtu operation,ina maana ana ufahamu mkubwa hata wa upatikanaji wa macho ya bandia ,unamuacha mgonjwa anatoka hospitali anaingia mtaani kuanza kuulizia watu wengine wakati yeye aliepo kwenye hiyo fani ndio angepaswa kuwa msaada mkubwa kwa mgonjwa.Hii sio nzuri,kutoka kwa jicho kungepaswa kuwepo na counciling ya hali ya juu sana ukichukulia kuwa halitarudi tena.
 
Pole sana mkuu, kuna mdau katoa namba za ccbrt, jitahidi uwatafte unaweza pata msaada.
 

Madaktari wetu wanawaza pesa tu ukiumia kidogo mguu hawaumizi kichwa wanakuanbia mguu ukatwe kusolve tatizo.

Mimi nina ndugu yangu aliamka na kujikuta jicho linauma kaenda ccbrt anaambiwa kuna kidonda ndani na kinazidi kuchimba kuelekea ndani zaidi hivyo wakashauri atolewe jasho.
Wakamtoa na hazikupita siku nyingi akafariki.

Sent from my Philips savy
I
 
hospital za bongo ni mungu anasaidia tu mkuu sijui shida ni nin

labda maslahi ni madogo au mifumo mibovu

nilikua na mgonjwa anatakiwa afanyiwe opareshn ya mguu hospital moja iv dodoma tulizungushwa wiki 2 mgonjwa anatolewa wodin anapelekwa chumba cha upasuaji madoctor wanamrudisha wodin kila siku tunaandikiwa tu vifaa vya kununua kumbe walkua wanataka laki 8 na nusu ndio wafanye opp vifaa vyote vilikuepo na mgonjwa ana bima
 
Pole sana,ila kikubwa uzima.....ngoja waje wanaojua ila unaweza kutumia miwani nyeusi kama haujisikii comfortable kutoka nje unavaa hiyo miwani,pole sana

Sent from my T1-701u using JamiiForums mobile app
hasante

Sent from my Magnus bravoZ10 using JamiiForums mobile app
 
Nenda CCBRT IPO msasani dar au nenda China wana ujuzi wa kuweka mboni ya nguruwe.

Sent from my HUAWEI CUN-L21 using JamiiForums mobile app
hasante kwa ushauri wako.je garama zao unazijua?samahan lakin kwa maswari meng

Sent from my Magnus bravoZ10 using JamiiForums mobile app
 
du jaman

Sent from my Magnus bravoZ10 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…