GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wanabodi, Mada hii ni kutokana na kongamano la kujadili siku Mia moja za Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Wasimamizi wa taasisi zote kwa kuzitaja TRA, Bandari, TCRA na Uhamiaji wamejitokeza kwenye kongamano huku wakisifu na kusema wametekeleza kauli, Matamko na hotuba za Rais Samia Suluhu Hassan kwa siku Mia moja na wameona tofauti na awamu iliyopita kwa kukusanya mapato mengi na kuacha watu wawe huru
Je?, kama nchi tunafuata katiba na sheria tulizoziweka au tunasimamia kauli za Rais, Hayati Magufuli alifanya mambo bila kufuata katiba wala sheria na mwisho wa siku ukajengeka ufalme kwa Rais kuikamata mahakama na Bunge. Watu wote ambao Rais Hayati Magufuli kwa mazingira ya kujificha aliweka mkono wa kuwahukumu kupitia mahakama kesi zao zinafutwa na Sasa Wengine wanarudishiwa Faini zao
Kama Rais ndio katiba na yupo juu ya katiba na sheria kwanini tuwe na Bunge na Mahakama, Rais anaweza kuilazimisha mahakama yaani majaji na Mahakimu kufuata atakavyo na kutenda atakayo, Ni muda muafaka kwa watakao anza kujadili katiba waufute muhimili wa mahakama kabisa na kuanzisha Mahakama ya Rais nchi nzima itakayotekeleza kauli za Rais na sio kuwa na mfumo wa mahakama kama sasa
Je? Bunge la Job Ndugai ni Bunge linalomilikiwa na utashi wa Rais au lipo kwa Katiba na Sheria, Kama ni Bunge la katiba kwanini linawakumbatia Halima mdee na wenzake ambao hawatakiwi kuwa Bungeni
Bunge la Job Ndugai limetumika kupora haki za wapinzani kama Tundu lissu kwa kuwa liliendeshwa kwa utashi wa Rais, Bunge lilitumika na kulazimishwa kupitisha sheria kwa utashi wa Rais na hili Job Ndugai mwenyewe anajishangaa na kushangaa kwanini Bunge aliloliongoza lilipitisha sheria za uhujumu Uchumi, uchochezi na kila aina ya vituko
Ni muhimu watakaojadili katiba mpya walifute Bunge la sasa na kuanzisha Bunge la Rais ambalo litatumika kupitisha Matamko, kauli na utashi wa Rais
Ni muda muafaka kuelimisha jamii kuhusu taratibu za nchi, Tunawalaumu watu kama Ole Sabaya na Paul Makonda kuwa walifuata utashi wa Rais na sio sheria na katiba, Yawezekana Sabaya na Makonda waliyafanya waliyoyafanya baada ya kuona Rais ndio katiba na Rais yupo juu ya sheria, Rais ana uwezo wa kuliamuru Bunge na kuilazimisha mahakama kufuata ngoma na mdundiko auchezao Yeye Rais na sio katiba na Sheria
Bila umakini wa katiba kila Rais atajifanyia atakalo kwa kisingizio cha Maendeleo, kujenga nchi au kujenga Uchumi huku akiminya uhuru wa Raia wa kisiasa na kukosoa
Mjadala wa katiba ni muhimu sana
#Katiba mpya kwa maslahi ya Tanzania mpya