SoC02 Je, Nchi yetu mali ya nani?

SoC02 Je, Nchi yetu mali ya nani?

Stories of Change - 2022 Competition

Mdaka Mdaka

Member
Joined
Jul 23, 2022
Posts
5
Reaction score
4
JE, NCHI YETU MALI YA NANI?

Nikiwa kijana niliyehitimu Elimu ya Chuo kikuu mwaka huu wa 2022 katika shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma. Nilitumia muda wangu mwingi kujifunza kuhusu jamii yangu, Nchi yangu, Bara langu na Dunia kwa ujumla, huku nikiamini elimu yenye manufaa, niutajiri usiofilisika.

Nimejifunza na kujielimisha ili nipate maarifa kwa ajili yangu binafsi na jamii yangu kiujumla, kwani ukikosa elimu yenye kukufaa, utabaki na ujinga unaokutesa. Sikuishia kusoma vitu vya darasani tu, bali pia navingi vyanje yadarasa maana niliamini elimu haina mwisho, hivyo hata muda wakujifunza huwa hautoshi sikuzote.

Nimepata majibu mengi juu ya mambo yaliyokuwa yakinitatiza, pia maswali mengi kwamambo niliyoya-dadavua. Sikutaka kujitengenezea majibu ya kipumbavu kwamaswali ya msingi, nidhahiri jibu lakijinga kwaswali sahihi nidalili za kushindwa. Badala yake nilichimba vyakutosha ili niweze kuvyonza maarifa naniwe miongoni mwa walioelimika.

Miongoni mwa maswali yaliyonitatiza sana ni, Je Nchi yetu Mali ya nani? Nijuavyomimi heshima ya msomi ni kuipigania jamii yake na kuchambua mambo yenye ukakasi. Hivyobasi hutakiwi kuogopa kusema kwani utakuja kusemwa na msemaji siku yakusema, akuseme kwanini haukusema naulikuwa nauwezo wakusema. Ndiomaana nadiriki kusema, Je Nchi yetu mali ya nani?

Nitajaribu kugusa sehemu muhimu tu, zitazotupa miguu yakusimamia. Nitaepuka kutoa maelezo mengi yasiyonatija. Lengokuu ni kufahamu, Je Nchi yetu Mali ya nani?

1: Nchi yetu ya Tanzania: Ibara ya 1 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema, "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano", ikiwa na maana eneo lenye Watu, Mipaka, Mamlaka huru na taasisi za kiutawala(Serikali). Namwisho ikayaweka mamlaka makubwa ya kimaamuzi katika taifa mikono mwawanachi ndani ya ibara ya 8.-(1)(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii. Je nikweli? Makala hii itajaribu kupekenyua.

2: Nchi yetu ilipotoka: Nchi yetu ya Tanzania imepitia nyakati mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa.

a》Katika historia ya binadamu, sisi Waafrika wa Tanzania na kwingineko barani Afrika, tumepitia madhila makuu matatu, ambayo ni ¹Utumwa, ²Ukoloni na sasa ³Ukoloni mamboleo. Utumwa ulituondolea utulivu na nguvukazi, Ukoloni ukatuondolea utu na mamlaka, Ukoloni mamboleo ukatutia unyonge na kupalilia umaskini uliopandwa zama za ukoloni.

b》Jitihada za kudai Uhuru zilishika kasi miaka ya 1950 na 1960. Kwaweledi wa wazalendo wataifa letu akiwemo Mwalimu Julius Nyerere Nchiyetu ikapata uhuru mwaka 1961, Nyerere akiwa Waziri Mkuu huku mamlaka yamwisho yakiutawala yakiendelea kubakia London. 1962 Nchi inakuwa Jamhuri, Nyerere anakuwa Rais, kwamaana sasa wananchi ndio wenyenchi. Muda mfupi baada ya hapo, Uhuru wa umma ukatoweka na kikundi kidogo cha watu(wanachama wa TANU) wakahodhi maamuzi ya Taifa, hiyo inamaanisha sasa wenyenchi ni TANU, kikundi cha watu wachache. Naikabaki hivyo kwa muda huku miradi, mipango na mikakati yakitaifa ikipangwa nawao. Mfano mzuri ni Azimio la Arusha(1967), unyumbuishaji wa Katiba n.k.

c》Kufuati anguko baya la kiuchumi miaka ya 1980, halingumu ya kimaisha na kufeli kwa Serikali ya Kiimra juu ya kukidhi mahitaji muhimu kwa taifa, taasisi za fedha za Dunia(Benki ya Dunia na Taasisi yafedha yakimataifa, IMF)zilikuja na tiba mbili, ¹Kufungua milango ya Uchumi(Liberalization) na ²kuuvunjavunja utawala wa kiimra(Decentralization) kama njia yakuchochea demokrasia na kuponya uchumi, ili kufuzu kupata msaada wa kifedha. Mudahuu wanaoshinikiza maamuzi ni taasisi za fedha zanje nasio wananchi wa Tanzania, Sio tume ya Nyarari wala Bunge la Jamhuri.

3: Nchi yetu ilipo: Kufuati kuingizwa kile wanachodai ni Demokrasia ya vyama vingi, chaguzi kadhaa zimefanyika zikiwemo chafuzi pia. Kupanuliwa kwa Asasi za Kiraia(AZAKI) na kuruhusu midomo ya watu kuongea.

a》Tumeshuhudia Mauaji ya Wazanzibar walioandamana kihalali kutetea kura zao, mauaji ya Wamasai wanaotetea Ardhi yao, kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na mtu mmoja, ufisadi wa kupindukia kama Escrow, EPA na Richmond,matumizi makubwa yafedha za Serikali pasi na ushirikishwaji( kama kununua Ndege, Treni ya umeme n.k), upotevu wakutatanisha wa fedha za umma( Mfano Tirioni 1.5, alizofichua CAG Assad), kuokotwa ufukweni kwa miili kwenye viroba ikiwa imekufa huku ikionyesha majeraha mabaya, watu kutekwa, kupotea, kupigwa risasi hadharani na hata kubambikiziwa kesi. Haya yote yanaibua swali gumu, Je Nchi yetu mali ya nani? Kama sisi ndio wenyenchi, mbona haya yanatufika? Kama ni bahatimbaya, mbona yanajirudiarudia?

b》Ukandamizaji mkubwa wa demokrasia, uvunjifu wa sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu, limekuwa jambo la kawaida kufanywa na watumishi wa Serikali, Vyombo vya dola(Polisi, Usalama Wataifa) n.k.

c》Ufujaji, ufisadi, ubadhirifu mkubwa wa mali yaumma tumeushuhudia huku hatua dhaifu zikichukuliwa, nahata mda mwingine kutetewa na kauli ya, "haikuwa mali ya Umma". Katika hotuba za kupokea ripoti za mchanga wa madini, Rais Magufuli alikili kuwepo hujuma kubwa Serikalini inayofanywa na Watanzania wachache wakishirikiana na wageni kwamaslahi yao binafsi. Serikalini sasahivi, rushwa, wizi na ufisadi unavutia kama sura ya Cleopatra.

d》Mhimili wa Mahakama sasahivi umebaki kuilinda Serikali. Mhimili wa Bunge leo ndio mtetezi mkuu wa Serikali, hupiga ngonjera zamapambo na nderemo zautukuzo huku lengo la uwakilishi na usimamizi likipotelea hewani kama moshi wa sigara.

4: Nchi yetu inapokwenda: Binafsi sijui wapi tunakwenda. Sijui tunaenda kuwa Malawi ya Kamuzu Banda au Yugoslavia ya Josip Broz Tito, ila nnatumaini moja kubwa yakuwa misukosuko ndio mwendo wa Ngarawa.

Hitimisho; Binafsi sijapata jibu mujarabu juu ya swali hili, maana huniletea majibu yenye suratatu kama sanamu lamiungu Yakihindu. Sura yakwanza huniambi, Nchi yetu nimali ya wachache walioko madarakani, wanaokula mema ya Nchi, keki ya Taifa na kufaidi fungate ya Uhuru. Sura yapili hunambia, nimali ya taasisi kubwa za fedha ambazo ndio wafadhili wakuu wa Nchi yetu, nakuthibitisha hilo rejea mchakato wa Structural Adjustment Program(SAP) na Watoto wakike waliopata mimba kurudi Shuleni baada ya kujifungua. Sura yatatu hunambia, nimali ya Mabepari-konkodi wenye mamlaka yakuipangia Dunia nini cha kufanya kama Marekani na baadhi ya mataifa makubwa ya Ulaya, namakampuni yao nyonyaji, nasasa kunakirusi-China kinaingia. Lakini Sio Mali ya Wananchi.

Kunanjia tatu kuu za kujibu swali. ¹swali kwa swali, ²swali kwa maelezo na ³swali kwa mkato. Nimejibu swali kwa maelezo nasasa najibu swali kwakuuliza swali, Je Nchi yetu mali ya nani?
 
Upvote 0
Nchi haiwezi kuwa Mali ya mtu nchi ni ya wenye nchi
 
Back
Top Bottom