Je, nchi zote raia wake husimama bendera inaposhushwa saa 12 jioni?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Swali linaeleweka wakuu naombeni kujuzwa najua JF wengi mmesafiri mambele huko; je, huko kuna taratibu za kushusha bendera na watu wakasimama kusubiri filimbi ipulizwe nchi za wenzetu huko?
 
Siyo nchi zote kwamba hushusha bendera zao saa 12 jioni.

Wengine ikipanda labda iende nusu mlingoti. Vinginevyo imechakaa ya kutupa.
 
Ile kushusha saa 12 maana yake nini,? Au haina maana.
 
Mkuu huu ni utamaduni tu uliozoeleka kwa baadhi ya nchi. Wengine wakidhani usiku bendera haionekani.

Kumbuka bendera yetu hushushwa hata mvua ya maana inapotaka kunyesha.

Bendera inapokuwa juu inatafsiriwa kuwa serikali iko kazini au iko macho.

Wasioshusha wanajiaminisha kuwa serikali huwa hailali na Iko kazini muda wote.

Mambo ya Imani tu mkuu.
 
Swali linaeleweka wakuu naombeni kujuzwa najua JF wengi mmesafiri mambele huko; je, huko kuna taratibu za kushusha bendera na watu wakasimama kusubiri filimbi ipulizwe nchi za wenzetu huko?
Kusimama ni swala la kizalendo ambalo hatuangalii mataifa mengine wanafanya nini, asiyependa ahamie Burundi. Binafsi Ile NIDHAMU ya kizarendo naipenda sana, mtu anayehoji hilo na ni mTanzania hana maana
 
Kumbe nchi inajitahidi kuvuta watalii wengi, na wengi wao hata hawajui bendera ya nchi wanakoenda ni ipi. Wasimame pia? Wapigwe? Wasipoelewa Kiswahili wala Kiingereza??
 
Swali linaeleweka wakuu naombeni kujuzwa najua JF wengi mmesafiri mambele huko; je, huko kuna taratibu za kushusha bendera na watu wakasimama kusubiri filimbi ipulizwe nchi za wenzetu huko?
Mimi ile ya kijani ikishushwaga nachuchumaa kabisa hadharani bila aibu na qunyer
 
Back
Top Bottom