Je, NI AINA GANI YA KODI INAYOTAKA KUTOZWA KWA KADI ZA SIMU??

Je, NI AINA GANI YA KODI INAYOTAKA KUTOZWA KWA KADI ZA SIMU??

Chagga King

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
1,866
Reaction score
1,076
[h=5].KHS KODI ZA KILA MWEZI KWA KADI ZA SIMU

..TULIWEKE HILI SUALA VIZURI, NA TUSIBURUZWE TU. KWA UFAHAMU WANGU MIMI NI KWAMBA KODI YA MAPATO HUWA INATOZWA PALE AMBAPO KUNA KIPATO ( INCOME) IWE KWA NAMNA YOYOTE ISIPOKUWA KWENYE MASHIRIKA YALIYOSAMEHEWA KODI, SASA HAPA TUJIULIZE SWALI, HIYO KODI TUTAKAYOKUWA TUNAILIPA KILA MWEZI, JE NI KWA KIPATO KIPI TUNAKIPATA KWA KUWA NA ILE KADI TU? , MAANA UTUMIE USITUMIE LAZIME UTOZWE HIYO KODI, JE NI KODI YA KUMILIKI LINE?, USAHIHI NI KWAMBA ILITAKIWA HIYO KODI ITOZWE MARA TU MTU ANAPONUNUA HIYO KADI YA SIMU, HII NI SAWA NA MTU ANUNUE BIDHAA ALAFU AILIPIE KODI KILA MWEZI (YAANI UNUNUE MFUKO WA SIMENTI LEO NA ULIPE KODI, ALAFU TENA BAADA YA MWEZI UULIPIE TENA KODI, SI UNAO), NADHANI HAPO HAKUNA UHALALI WOWOTE WA HIYO KODI, KAMA NI KODI YA MTU KUFANYA MAWASILIANO, MBONA HUWA TUNAILIPA PALE TUNAPONUNUA MUDA WA MAONGEZI KWA SABABU ILE VOCHA HUWA INAJUMUISHA VAT (kuna sehemu kwenye vocha pameandikwa VAT INCLUSIVE), MIMI NAAMINI TUKIWAULIZA HAWA TRA NA TCRA NI KITU GANI HASA KATIKA KADI YA SIMU TUNACHOKILIPIA KODI (KATI YAUMULIKI WA KADI NA KUTUMIA HIYO KADI) HAWATAKUWA NA JIBU SAHIHI. MAANA UMULIKI WA KADI, KODI YAKE TUNAILIPA MARA TUNUNUAPO KADI, NA KAMA NI MATUMIZI YA KADI BASI KODI YAKE TUNAILIPA PALE TUNAPONUNUA HIYO VOCHA, MAANA KADI YA SIMU HAIWEZI TUMIKA KAMA HAINA MUDA WA HEWANI, LABDA UPIGIWE. NA INAONEKANA TRA WENYEWE WAMESAHAU KUWA WANA SERA YA KWAMBA KODI ILIPWE PALE KUNAPOFANYIKA TRANSACTION, SASA HIYO TUTAKAYOILIPA KILA MWEZI NI KWA TRANSACTION GANI.

TUWE WAUNGWANA.
[/h]
 
mkuu hii ni head tax lisikuchanganye jina ilo
 
Kodi sio lazima ulipe ukipata kipato tu. Kunaaina nyingi ya kodi. Mfano VAT unalipia ukinunua bidha au ukipata huduma. Hata health insurance nayo ni kodi, kwa wale wafanyakazi wa serikalini wanakatwa kila mwezi.
Excise duty unalipia ukinunua bidhaa fulani ambazo zimetakiwa kulipia hii kodi au huduma mfano money transfer kwa bank au simu. Mara nyingi hakuna sababu maalum ya kutoza excise duty katika hizo bidhaa. Hii kodi inatozwa kwenye maji, juice, pombe, soda, vocha etc. Pia hii hiyo kodi ya sim card nayo ilitozwa kupia sheria ya excise duty. Hii ni njia tu ya serikali ya kukusanya mapato.
 
...thanx ndugu, lakini mbona naona kama computation ya hiyo kodi haipo fair, 1000 kwa mwezi wametumia kigezo gani kupata hiyo 1000/month? mfano VAT ni 18% katika price ya goods or services, kwenye umiliki wa kadi je?
 
Kunanjia nyingi za kutoza kodi. Sio lazima kodi iwe charged at rates mfano hiyo VAT au excise duty.
As i said before kama health insurance kwa wafanyakazi wa serikalini ambao wanakuwa tax a specific amount every month.
So hata hiyo kodi ya kadi za simu inaweza kutozwa kwa aina hiyo.
 
Kuongea hii ni mass taxes. Ni njia nzuri ya kukusanya kodi ambayo serikali nyingi zinaitumia. Kodi inakuwa inatozwa kwa kiasi kidogo sana labda kila mwezi. Labda shilingi mia au mia mbili. Kitu ambacho mtu haoni shida kulipia. Sasa hawa tanzania wamepitiliza na hiyo 1000 yao. Ambayo its too much.
 
.. taxbabe, thanx much, and its good thing that u don't support the amount
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom