je ni bank gani inayotoa huduma ya paypal account?

Rapunzel

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Posts
1,079
Reaction score
599
habari zenu wadau!
naomba kufahamishwa ni bank gani inayotoa huduma ya paypal account na process zake zikoje?
asanteni.
 
Nadhani zote zinazosupport VISA na MASTER CARD. Uhakika, mie natumia account ya CRDB ambayo nimelink na paypal. Process zao si ngumu:
1. Nenda bank ya CRDB omba fomu ya kuunga card online. Jaza hapo hapo kisha subiri ndani ya 24hrs inawezeshwa.
2. Fungua paypal account (kama huna). Kisha fanya process za kuunga card yako na paypal, verify.
3. Subiri siku 3-5, nenda bank chukua statement. Utakuta secret code imetumwa. Ingiza kwenye account yako ya paypal.
4. Anza kufanya manunuzi kwa fujo.
 

nashukuru sana kwa kunifahamisha
 
exim bank wanatoa hii huduma kwa kutumia silver card au gold card
 

Kuna gharama zozote za kufungua hiyo paypal?ni kiasi gani?
 

Nafikiri

4. weka pesa ya kutosha kwenye accout yako, halafu 5. iwe hiyo kwenye red
 
Nafikiri

4. weka pesa ya kutosha kwenye accout yako, halafu 5. iwe hiyo kwenye red

Si lazima hata kidogo. Paypal inafanya transaction moja kwa moja kutoka kwenye account yako halisi kwenda kule utakako. Hawahifadhi pesa zako labda kama ni malipo yanafanyika kwenye akaunti yako ya paypal, lakini si wewe kutumia credit card kuhifadhi pesa zako paypal. Unapofanya manunuzi hakikisha tu kwamba unapesa kwenye akaunti yako halisi.
 

ndio inabidi ajaze pesa ya kutosha kwenye hiyo uliyoiita account yake halisi kabla ya kufanya manunuzi kwa fujo, au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…